MATI SUPER BRANDS YADHAMINI MAONESHO YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR 2024 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, August 9, 2024

MATI SUPER BRANDS YADHAMINI MAONESHO YA TANZANITE MANYARA TRADE FAIR 2024



Na Mwandishi Wetu ,Manyara .


Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi kupitia kinywaji chake pendwa cha Tanzanite Premium Vodka imedhamini Maonesho ya tatu ya Biashara,Viwanda na Kilimo ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 yatakayofanyika katika Viwanja vya Tanzanite Kwaraa Stedium Octoba 20-30 mwaka 2024 mjini Babati Mkoani Manyara.

Kwa Upande Wake Afisa Masoko Kampuni ya Mati Super Brands Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo imeamua kudhamini maonesho hayo ili kuunga mkono jamii ikiwemo wajasiriamali wadogo na wakati kupata fursa ya kujitangaza kupitia maonesho hayo.

Kauli mbiu ya maonesho hayo ni "Manyara kwa ustawi wa biashara na uwekezaji "

No comments:

Post a Comment