MENEJA ya Idara ya Mipango wa Wakala.ya Barabara Tanzania (TANROADS), Makao Makuu Mhandisi Arnold Masaki,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
Na Okuly Julius -DODOMA
MENEJA ya Idara ya Mipango wa Wakala.ya Barabara Tanzania (TANROADS), Makao Makuu Mhandisi Arnold Masaki amesema kwenye mikataba ya ujenzi wa barabara nchini wanayoingia na wakandarasi vipo vipengele vinavyowataka kupanda miti, katika barabara zote zinazojengwa.
Mha. Masaki amesema katika maeneo ambayo umefanyika ujenzi wa barabara wamezingatia upandaji miti kwa mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Mhandisi Masaki ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni jijini Dodoma.
Amesema kuwa upandaji miti huo ni muendelezo wa shughuli mbalimbali ambazo wanazifanya zikiambatana na maonesho katika banda lao lililopo kwenye viwanja vya Nzuguni, na kwamba wamepanga miti 100 kuzunguka jengo hilo la ofisi, pamoja na barabara ya Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuleta madhari nzuri katgika eneo hilo.
Kuhusu makandarasi alisema vipo vipengele vinavyowataka kuzingatia upandaji wa miti kandokando ya barabara kabla au baada ya kukamilisha ujenzi ili kuzuia mmomonyoko na kuifanya miji ipendeze kwa kuwa ya kijani.
Naye Meneja wa Mizani wa TANROADS, Mhandisi, Leonard Mombia,ametoa wito kwa watumiaji wa barabara nchini wakiwemo madereva kutunza, kuheshimu na kuthamini alama za barabarani na vivuko maana alama hizo zimewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji.
"Alama na vivuko hivyo tukivitunza na kuviheshimu vitatusaidia sisi sote wakati wa kutumia barabara hizo na kuepusha ajali ambazo zinaweza kujitokeza kutokana na ukiukaji wa matumizi ya barabara hizo,"alisistiza Mhandisi Mombia.
Meneja huyo akizungumza uzagaaji na upitishaji wa mifugo kwenye barabara alisema, si jambo jema maana barabara hizo zimejengwa ili kurahisisha usafiri na usafirishaji hivyo kuacha mifugo ilirandaranda hovyo kunasababisha kupunguza uimara wa barabara husika na kuzuia ukuaji wa uchumi na kutofikiwa kwa malengo endelevu.
Awali mwananchi aliyeshiriki katika shughuli hiyo ya upandaji miti, Said Muome, alipongeza TANROADS kwa kutekeleza jukumu hilo kutokana na umuhimu wa miti wa kusaidia kutunza mazingira na kuweka madhari nzuri kando ya barabara na majengo.
MENEJA ya Idara ya Mipango wa Wakala.ya Barabara Tanzania (TANROADS), Makao Makuu Mhandisi Arnold Masaki,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
MENEJA wa Mizani wa TANROADS, Mhandisi, Leonard Mombia ,akizungumza na waandishi wa habari mara ya zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
WATUMISHI wakiendelea na zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
MENEJA ya Idara ya Mipango wa Wakala.ya Barabara Tanzania (TANROADS), Makao Makuu Mhandisi Arnold Masaki,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
MENEJA wa Mizani wa TANROADS, Mhandisi, Leonard Mombia ,akizungumza na waandishi wa habari mara ya zoezi la upandaji miti katika jengo la TANROADS Makao Makuu linaloendelea kujengwa katika eneo la Njedengwa jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa shughuli za Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa zinazofanyika eneo la Nzunguni.
No comments:
Post a Comment