WIZARA YA FEDHA YAPAMBA MAONESHO YA NANE NANE - DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, August 4, 2024

WIZARA YA FEDHA YAPAMBA MAONESHO YA NANE NANE - DODOMA

Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Mary Mihigo (kulia), akitoa maelezo kwa mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Raphael Enock, kuhusu elimu ya fedha ya namna ya kuweka akiba, usimamizi wa fedha binafsi na namna ya kujipanga na maisha ya uzeeni, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika Kitaifa katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Tehama Mwandamizi, Idara ya kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Zaina Mwanga (kulia), akimwelekeza Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Godfrey Msambwa, namna ya kupakua Application ya GePG inayorahisisha kulipia malipo ya huduma za Serikali, wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Fronto Furaha (kulia), akiwaelezea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Marie De Mathias ya jijini Dodoma, kuhusu majukumu ya Wizara hiyo katika kusimamia Uchumi, wakati walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Mkazi wa jiji la Dodoma, Bw. Ramadhan Mbalamwezi (Kushoto) akiScan Msimbo wa QR yenye maelezo kuhusu Mfumo wa Hazina ya Machapisho wa Wizara ya Fedha, wakati alipotembelea Banda la wizara ya hiyo, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”. Kulia ni Afisa Maktaba Mwandamizi kutoka Wizara hiyo, Bw. Tumaini Katabazi.
Afisa Sheria kutoka ⁠Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Amosi Ndegi (kulia), akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Taifa wa Ununuzi (NeST) kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma, waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Afisa Habari Mwandamizi, kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Farida Ramadhan (kulia), akiwaelezea wanafunzi wa Shule ya Sekondari Marie De Mathias ya jijini Dodoma, kuhusu huduma zinazopatikana katika Banda la Wizara, wakati walipotembelea katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya Nane Nane, Nzuguni, jijini Dodoma, yaliyobeba kaulimbiu ya “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)

No comments:

Post a Comment