ZAIDI YA HEKTA LAKI NNE HUPOTEA KUTOKANA NA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, August 24, 2024

ZAIDI YA HEKTA LAKI NNE HUPOTEA KUTOKANA NA MATUMIZI YA KUNI NA MKAA

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (wa katikati) akiwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Mdahalo wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 23, 2024. .PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kulia) akizungumza na mdau wa Nishati Safi ya Kupikia katika mabanda yaliyowekwa nje ya ukumbi mkutano ambao Mdahalo wa Nishati Safi ya Kupikia ulikuwa ukifanyika Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 23, 2024. PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Husnuu Makame iliyopo Kibuteni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja alipotembelea shuleni hapo kuona namna shule hiyo inavyotumia mfumo wa Nishati Safi ya Kupikia. PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kushoto) akimsikiliza Mkuu mkuu wa Shule ya Shule ya Sekondari ya Husnuu Makame Mwl. Issa Ali Ali iliyopo Kibuteni Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja alipotembelea shuleni hapo kuona namna shule hiyo inavyotumia mfumo wa Nishati Safi ya Kupikia. PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS


Na Mwandishi Wetu


Hekta zaidi ya laki nne za misitu hupotea kila mwaka kutokana na matumizi yasiyoendelevu ya rasilimali za misitu ikiwemo uvunaji wa miti kwa ajili ya kuni na mkaa.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme katika Mdahalo wa Nishati Safi ya Kupikia uliofanyika Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 23, 2024. 

Amesema hali hii imekuwa ikisababisha madhara makubwa ikiwemo kupungua kwa vyanzo vya maji, kuwepo kwa vipindi virefu vya ukame na kupoteza bioanuai.

“Matumizi ya kuni na mkaa huchangia katika uchafuzi wa hali ya hewa kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa gesi joto na kuongezeka kwa viwango vya joto, kupungua kwa viwango vya hewa safi ya oksijeni inayozalishwa na miti, na uharibifu wa tabaka la Ozoni.

Hata hivyo, Bi. Mndeme amesema kwa mujibu wa mwongozo wa Benki ya Dunia kuhusu Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2020, nishati safi ya kupikia hupimwa kwa ufanisi, urahisi wa kutumia, upatikanaji, unafuu, urahisi wa kutumia, usalama na yenye kiwango kidogo cha sumu.

“Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kama vile gesi (LPG) au majiko ya umeme hupunguza moshi unaotokana na kuni na mkaa ambao unaweza kusababisha magonjwa ya kupumua kama vile pumu na saratani.

“Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia yatanufaisha wanawake na watoto ambao mara nyingi hutumia muda mwingi jikoni na kuepuka athari za muda mrefu za kuvuta moshi,” amesema Bi. Mndeme.
Ameongeza kuwa utumiaji wa Nishati Safi ya Kupikia yanapunguza kasi ya ukataji miti kwa ajili ya kuzalisha mkaa na matumizi ya kuni, hivyo Nishati Safi husaidia kuhifadhi misitu, kupunguza mmomonyoko wa ardhi na kupunguza uzalishaji wa gesi joto.

“Ingawa gharama za awali za kununua vifaa vya nishati safi zinawea kuwa juu, lakini matumizi ya nishati hiyo ni ya muda mrefu, hivyo ni nafuu ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Asemema sekta ya Nishati Safi inatoa fursa ya ajira kwa maeneo kama usambazaji wa gesi na utengenezaji wa majiko sanifu ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment