APANDISHWA KIZIMBANI KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI YAKIWEMO UBADHIRIFU NA UFUJAJI WA FEDHA ZA TCCIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, September 24, 2024

APANDISHWA KIZIMBANI KWA MAKOSA YA UHUJUMU UCHUMI YAKIWEMO UBADHIRIFU NA UFUJAJI WA FEDHA ZA TCCIA


Bw. Gotfrid Mutagwaba Muganda aliyekuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), amefunguliwa
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 27108/2024 na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Septemba 23, 2024.

Shauri hili limefunguliwa mbele ya Mhe. Anneth Nyenyema - Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Wilaya Ilala.

Mshtakiwa ameshtakiwa kwa makosa mawili yakwemo; Ubadhirifu na Ufujaji wa sh. 39,894,000/= mali ya TCCIA pamoja na kosa la matumizi mabaya ya madaraka kinyume na kifungu cha 28(2) na 31 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (Sura 329 Rejeo 2022).

Shauri hili lilitokana na tuhuma dhidi ya mshtakiwa kumpatia ajira Ms.JANETH KAMBONA kwa nafasi ya Msaidizi Binafsi wa Rais wa TCCIA, huku akijua ni kinyume na utaratibu.

Mshtakiwa amekana makosa yote na kupelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana aliyopewa.

Shauri limeahirishwa hadi Oktoba 7, 2024
kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa Hoja za Awali.

TAKUKURU Ilala, Septemba 23, 2024.

No comments:

Post a Comment