Septemba 24, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, mbele ya Mh Herrieth Mhenga, limefunguliwa shauri la jinai Na 27222/2024 dhidi ya Jumanne Ramadhani Mhando - Mkusanya Ushuri Halmashauri ya Wilaya Siha.
Mshtakiwa anakabiliwa na makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni kosa la rushwa kinyume na kifungu cha 15 (1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (sura ya 329) na kosa la pili ni kosa la kukaidi kutekeleza jukumu la kisheria kinyume na kifungu cha 123 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura 16 marejeo ya mwaka 2019.
Mshtakiwa alijipatia kiasi cha shilingi 2,925,350/= ikiwa ni manufaa yaliyotokana na ushuru aliokusanya kwa kutumia mashine ya poss.
Aidha mshtakiwa alikana makosa yote na yupo nje kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya damana.
Shauri hili litakuja kwa masikilizo ya awali tarehe 15.10.2024
TAKUKURU KILIMANJARO.
No comments:
Post a Comment