FANYA UFANYAVYO, LALAMIKA UWEZAVYO, LAKINI ELEWA KUWA,,,, - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 25, 2024

FANYA UFANYAVYO, LALAMIKA UWEZAVYO, LAKINI ELEWA KUWA,,,,


CHANZO NI RSA TANZANIA

1. Sheria inakataza kuovateki mahali mistari inapokataza kuovateki na wala haijasema ikiwa mbele kweupe (clear) overtake. Kuamua kuovateki ni akili na utashi wako mwenyewe tu (s.50);

2. Sheria inataka kila dereva kusimama kwenye kivuko cha waenda kwa miguu kuwapisha wavuke, awe mvukaji ni mmoja au kundi (s.65(10));

3. Sheria inakataza kushabikia mwendokasi (overspeeding) au kumchochea dereva kukiuka sheria;

4. Sheria inakataza kwenda mwendo wa zaidi ya 50kph kwenye maeneo ya makazi na yenye mwendo kikomo wa 50kph na nje ya hapo gari la uzito wa zaidi ya tani 3.5 haliruhusiwi kuzidi spidi 80kph (s.51(8));

5. Sheria inakataza dereva wa basi au lori kuendesha huku akiwa amekunywa pombe na kwa gari nyinginezo pombe atakayokuwa amekunywa dereva isizidi 0.80mg/100mls za damu;

6. Sheria inakataza kuendesha gari bovu au kuruhusu gari bovu kuendeshwa barabarani (s.39(1)&(5));

7. Sheria inakataza kuzidisha abiria zaidi ya idadi iliyotajwa kwenye kadi ya gari;

8.Sheria inataka kila abiria kwenye gari apewe tiketi halali kutokana na gharama za umbali anaosafiri;

9. Sheria inataka dereva na abiria wafunge mkanda na kwenye pikipiki wavae helmeti (s.39(11)&(12)

10. Sheria inataka dereva kuwa na leseni halali muda wote akiwa anaendesha gari. (S.19&77)

11. Sheria inamtaka dereva atembee na kadi ya gari halisi au "certified."

12. Sheria inataka gari analoendesha dereva kuwa na bima wakati wote. (S.4 MVIA)

13. Sheria inamtaka dereva kutovuka taa nyekundu na aheshimu alama zote za barabarani kadiri zilivyosimikwa na Mhandisi wa Barabara.

Sheria ya mambo tajwa hapo juu haijawahi kubadilika tangu ilipotungwa. Hivyo ukitenda makosa hayo hapo juu na usikamatwe jua hiyo ni bahati yako tu siku hiyo hujapatikana, ila ukikamatwa utaadhibiwa na wala hupaswi kulalamika.

RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE

No comments:

Post a Comment