BODABODA WAUNGANA NA RPC KATABAZI KUKEMEA UHALIFU DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, September 23, 2024

BODABODA WAUNGANA NA RPC KATABAZI KUKEMEA UHALIFU DODOMA


Maafisa usafirishaji abiria kwa kutumia pikipiki maarufu (Bodaboda) wa kata ya Hazina wameahidi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma na kujiunga na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kukabiliana na uhalifu.

Kauli hiyo imetolewa September 23, 2024 na Maafisa hao Wakati wakizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP George Katabazi ambapo ametoa elimu ya ulinzi na ukamataji usalama.

Aidha Katabazi amewataka baadhi ya Maafisa hao kutokujichulia sheria mkononi pindi uhalifu unapotokea na badala yake kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kuchukua hatua stahiki kwa wahalifu.

Katabazi amewaasa maafisa hao kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana kwa pamoja kuzuia uhalifu na kuendelea kuulinda Mkoa wa Dodoma kwa kushiriki katika masuala ya ulinzi na kukemea uhalifu uliyopo katika jamii.

Toka Dawati la Habari Polisi Dodoma.

No comments:

Post a Comment