MAWAZIRI BASHUNGWA, LUKUVI NA CHANA KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA IRINGA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 21, 2024

MAWAZIRI BASHUNGWA, LUKUVI NA CHANA KUSHUHUDIA UTIAJI SAINI UJENZI WA BARABARA IRINGA.


Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera na Uratibu William Lukuvi, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana, wamewasili katika viwanja vya Samora kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Iringa - Msembe yenye urefu wa kilometa 104 kwa kiwango cha lami leo tarehe 21 Septemba, 2024.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi, Wabunge pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Peter Serukamba.

No comments:

Post a Comment