NAIBU WAZIRI MHE.SANGU AVIPIGIA CHAPUO VIKUNDI VYA TASAF MIKOPO YA HALMASHAURI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, September 21, 2024

NAIBU WAZIRI MHE.SANGU AVIPIGIA CHAPUO VIKUNDI VYA TASAF MIKOPO YA HALMASHAURI


Na.Lusungu Helela-Tabora


Naibu Waziri,  Ofisi ya Rais,  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu amezielekeza Halmashauri Mkoani Tabora kutoa kipaumbele kwa vikundi vya akiba na mikopo vinavyoundwa na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika utoaji wa mikopo. 

Mhe. Sangu ametoa maelekezo hayo leo  alipokuwa akitembelea miradi ya TASAF katika Kata ya Ipuli wilayani Tabora mkoani humo.

Amesema vikundi hivyo vinastahili kupewa mikopo kwa kuwa vimepewa elimu ya ujasiriamali kupitia TASAF na vimehakikishwa kuwa na nidhamu katika ukopaji na ulipaji.

Amefafanua kuwa mikopo ya asilimia kumi ambayo hutolewa na Halmashauri kote nchini huku akizitaka Halmasjauri hizo  zifanye kazi kwa kushirikiana na TASAF ili zijifunze jinsi ilivyofanikiwa katika suala la utoaji mikopo kwa vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana 

Amesema TASAF inasaidia walengwa wake kuanzisha na kuendesha vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana na kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali ii kukuza uchumi wa kaya zao.

Akizungumzia mpango wa Ajira za  muda kwa Walengwa, Mhe. Sangu amesema kuwa mpango huo si tu unatoa ujira na kusaidia kupunguza umaskini, bali pia ni fursa kwa walengwa kujifunza ujasiriamali na ufundi ambao huwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Hata hivyo Mhe. Sangu amepiga marufuku utaratibu wa kazi za ajira za muda kwa makundi yafuatato ikiwemo   wazee wenye zaidi ya  miaka 65 na kuendelea, watoto chini ya miaka 18 na akina mama wajawazito pamoja na watu wenye ulemavu.

Aidha, Mhe.Sangu amezitaka kaya za walengwa ambazo zina vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wana vigezo vya kujiunga na masomo ya elimu ya juu kutoa taarifa TASAF ili wapewe barua kwa uambatanisha na maombi ya mkopo ili aweze  kupata  mkopo huo kwa  asilimia 100.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paul  Chacha amesema ujio wa  TASAF katika Mkoa wake imeleta mapinduzi makubwa kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo wanufaika 13,467 wamewezeshwa kujiunga na Bima ya Afya Iliyoboreshwa (CHF), kuboresha makazi na kuanzisha vikundi vya kukopeshana.

No comments:

Post a Comment