Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka watumishi wa Sekta ya Maji kujifunza zaidi mambo mapya ili kujenga weledi na kuongeza uwezo wa kuhoji masuala mbalimbali.
Amesema hayo akifunga mafunzo kuhusu Ununuzi na Menejimenti ya Mikataba, jijini Dodoma.
Amewataka watumishi wa Sekta ya Maji kuongeza umakini katika kusimamia ubora wa kazi na kuepuka kufanya kazi kwa ubinafsi.
Mhandisi Mwajuma amewataka watumishi kutokubali kushindwa katika kusimamia mikataba ya kazi.
Amesema mafunzo hayo yatendewe haki na kila mtumishi kwa nafasi yake kwa sababu sio kila mtu hupata fursa ya mafunzo kama hayo.
No comments:
Post a Comment