Na Carlos Claudio, Dodoma.
Jeshi la Poisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watuhumiwa wanne wanaohusika katika matukio manne ya mauaji yaliyotokea kwa nyakati tofauti katika jiji la Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma SACP George Katabazi amesema watuhumiwa hao ni Paulo Daudi Mwaluko mwenye umri wa miaka 22 mkulima mkazi wa Mtumba, Isack Richard mwenye umri wa miaka 24 mkulima mkazi wa Mtumba, Erest Richard mwenye umri wa miaka 18 mkulima mkazi wa Mtumba na Silvanus Shotoo mwenye umri wa miaka 21 mkulima pia mkazi wa Mtumba.
Amesema tukio la kwanza ni tukio lililotokea usiku wa tarehe 1, Julai 2024 katika eneo la Mahomanyika Nzuguni ambapo waliuawa mabinti wawili ndani ya grosari waliokuwa wakifanya kazi kisha miili yao kuchomwa na moto.
“Tukio la pil lilitokea Agosti 28 2024 eneo la Mbuyuni Kizota ambapo aliuawa mwanaume mmoja na mke wake alijerehiwa na watoto wake watatu kisha godoro walilokuwa wamelalia kuchomwa moto ili waungue,”
“Tukio la tatu ni ambalo limetokea Septemba 6, 2024 huko eneo la Mkoze ambapo mama mmoja na mtoto wake waliuawa, tukio la nne liloitokea Septemba 16, 2024 huko katika mtaa wa Segu Bwawani Nala ambapo mabinti watatu waliuawa na kuchomwa moto na mama mawenye nyumba alijeruhiwa.” amesema Katabazi.
Aidha Katabazi amesema uchunguzi umebaini kuwa katika matukio yote hayo watuhumia wakishapiga kwa kitu kizito wanaowakuta kwenye nyumba waliovamia huwafanyia vitendo vya udhalilishaji
kisha kuchoma moto ili ionekane ni shoti ya umeme imetokea.
Sambamba na hayo Katabazi ameeleza kuwa uchunguzi zaidi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashukuru wananchi kwa ushirikiano wao uliofanikisha kukamatwa kwa mandao huo wa mauaji.
No comments:
Post a Comment