Na Said Njuki, Arusha
WAKATI Uchaguzi Serikali za Mitaa ukitarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu serikali imezidi kutoa mwongozo, huku ikisisitiza kuwa taratibu zote za uchaguzi huo zitafuatwa.
Akielezea mwongozo huo kwa viongozi wa mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa wa Halmashauri ya Meru wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha juzi, Msimamizi wa uchaguzi huo Zainab Makwinya alisema lengo ni kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa uwazi, haki na usawa.
"Mwongozo na utaratibu wa uchaguzi umetoka leo lengo ni kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uwazi, haki na usawa sanjari na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa". Alisema Makwinya.
"Haya ni maelekezo yanayofafanua kwa uwazi hatua kwa hatua mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia uandikishwaji na urejeshaju wa fomu za wagombea, uteuzi, lakini pia tarehe ya siku ya uchaguzi". Alisisitiza Makwinya ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru.
Alifafanua kwamba wagombea watakaoruhusiwa kugombea nafasi mbalimbali ni watanzania wenye umri usiopungua miaka 21, huku umri wa wapiga kura ukiwa ni miaka 18 na kuendelea ambapo fomu za wagombea zitaanza kutolewa Novemba mosi hadi saba mwaka huu ambapo uteuzi ikikamilika Novemba 10.
Akizungumzia mwongozo huo msimamizi wa uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi huo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Selemani Msumi aliwataka wananchi wenye sifa za ushiriki kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo kuhakikisha wanajitokeza kuanzia mwanzo hadi mwisho.
"Ni vizuri watu wote wakishiriki katika mchakato huo ili kukuza demokrasia nchini, lakini pia kuhakikisha wanapatikana viongozi bora watakaopigania maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla". Alisema Msumi.
Kwa mujibu wa mwongozo huo uliotolewa na serikali Septemba 26 mwaka huu kote nchini, ikiwa ni siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi lengo ni kuwapata Wenyeviti wa Mitaa, wajumbe watano wa Kamati za Mitaa katika Mamlaka za miji na vijiji nchini.
No comments:
Post a Comment