Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na watumishi pamoja na makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma akiwa katika jengo jipya la tume hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, wakati wa Maadhimisho ya siku ya tume yaliyofanyika kwa kupanda miti na kufanya matendo ya huruma.
Watumishi pamoja na makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) katika ukumbi wa jengo jipya la tume hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma, wakati wa maadhimisho ya siku ya tume yaliyofanyika kwa kupanda miti na kufanya matendo ya huruma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimwagilia mti alioupanda katika jengo jipya la Tume ya Utumishi wa Umma Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya tume.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akimkabidhi funguo ya bajaji mtumishi mwenye mahitaji maalum Bw. Enos Mtuso iliyotolewa na uongozi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakati wa maadhimisho ya siku ya tume, ikiwa ni utekelezaji wa mwongozo wa huduma kwa watumishi wa umma wenye ulemavu wa mwaka 2008.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa amepanda bajaji aliyoikabidhi kwa mtumishi mwenye mahitaji maalum wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Enos Mtuso, ikiwa ni utekelezaji wa mwongozo wa huduma kwa watumishi wa umma wenye ulemavu wa mwaka 2008.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samaria (hawapo pichani) kilichopo Hombolo mkoani Dodoma kabla ya kufanya matendo ya huruma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya tume.
Wakazi wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo mkoani Dodoma wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola (hayupo pichani) kabla ya kupokea misaada kutoka kwa watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma waliyoitoa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya tume.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola akikata utepe kuzindua vyoo alivyovikabidhi kwa wakazi wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyofanywa na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji mst. Hamisa Kalombola akisisitiza utunzaji wa vyoo alivyovikabidhi kwa wakazi wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyofanywa na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Muonekano wa vyoo vilivyokabidhiwa kwa wakazi wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyofanywa na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji (Mst.) Hamisa Kalombola akikabidhi misaada ya chakula, vifaa vya usafi na mavazi wa vyoo kwa wakazi wa kijiji cha Samaria kilichopo Hombolo mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya matendo ya huruma yaliyofanywa na Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma.
Na. Mwandishi wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, kuendelea kushiriki masuala ya kijamii ili kujenga mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka.
Mhe. Simbachawene ametoa maelelekezo hayo jijini Dodoma katika siku ya tume ambayo maadhimisho yake yameenda sambamba na kufanyika kwa matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji pamoja na upandaji wa miti katika jengo la Tume ya Utumishi wa Umma lililopo katika mji wa serikali Mtumba.
“Mmefanya jambo jema kumpatia bajaji mwenzetu mwenye mahitaji maalumu na mmeahidi kumuwekea mafuta, pia mmesema mnaenda Hombolo kutoa msaada kwa wenye uhitaji katika kituo cha wazee wa Samaria” Mhe. Simbachawene ameeleza.
Mhe. Simbachawene amefafanua kuwa, kitendo cha Tume ya Utumishi wa Umma kufanya hayo yote ni ishara ya upendo na ni matendo yanayompendeza Mungu na kumfariji mwanadamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Jaji mst. Hamisa Kalombola, wakati akikabidhi vyoo vilivyojengwa kwa ajili ya wenye uhitaji katika kijiji cha Samaria amewasihi wanufaika kuvitunza na kuzingatia usafi ili vidumu.
“Kuna methali inasema, vitunze vidumu kwahiyo maana yake hata mkiwa na vyoo mia mbili lakini msipovitunza havitadumu” Jaji mst. Kalombola amesisitiza.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wanufaika wenzie, mzee Antony Cyprian ameushukuru uongozi na watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kuwapatia msaada wa kuwajengea vyoo, ambavyo vimetatua changamoto waliyokuwa wakikabilina nayo.
Akizungumza kwa niaba ya Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Umma, Afisa Tawala Mwandamizi Bi. Dina Moshi amesema ushirikiano waliokuwanao umewawezesha kutoa msaada wa vyakula, vifaa vya usafi pamoja na mavazi wenye samani ya zaidi ya shilingi milioni tatu na kuongeza kuwa kiasi cha zaidi ya milioni 13 kimetumika kujenga vyoo nane.
Tume ya Utumishi wa Umma imeadhimisha siku ya tume kwa kupanda miti na kufanya matendo ya huruma, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment