TAMASHA LA UTAMADUNI 2024 KUFANYIKA MKOANI RUVUMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 11, 2024

TAMASHA LA UTAMADUNI 2024 KUFANYIKA MKOANI RUVUMA


Serikali imeandaa tamasha la utamaduni litakalofanyika mkoani Ruvuma, ambapo pamoja na kuenzi utamaduni litaleta faida nyingi za kiuchumi na litakalowavutia washiriki toka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani,linalotazamiwa kuwa na washiriki zaidi ya elf 16 ambapo Mgeni Rasimi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jumahuri ya muungano wa Tanzania Dkt: Samia Suluhu Hassan.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema tamasha hilo limebeba kauli mbiu ya"
"Utamaduni wetu ni utu wetu tuuenzi na kuuendeleza, kazi iendelee'

Tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 20 hadi tarehe 23 mwezi huu ambapo ametaja madhumuni ya tamasha hilo kuwa ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania, kuchochea ukuaji wa uchumi wa Nchi, kupitia ukuzaji wa sekta za ubunifu na utamaduni kutoa jukwaa la kuonesha kama msukumo madhubuti na utangamano wa Kitaifa kwa kuwaleta na kuwaunganisha wadau na viongozi wa sekta.

Kuendeleza na kuenzi urithi wa utamaduni na kutoa fursa ya majadiliano ya kitaaluma baina ya wananchi wa kila Mkoa, pamoja na kutumia kama nyenzo za kuenzi na kukuza utambulisho wa Kitaifa.

Msigwa amesema kuwa matamasha hayo ni maelekezo ya Mh Rais ambaye alielekeza wizara kuandaa matamasha hayo kila mwaka ambapo mwaka juzi lilifanyika Mkoani Dar es Salaam na mwaka jana lilifanyika Mkoani Njombe na mwaka huu linafanyika Mkoani Ruvuma.

Msigwa ameongeza kuwa kutokana na umuhimu wa tamasha hilo amewaomba asasi na taasisi zinazotoa huduma mbalimbali na washirika wa maendeleo makampuni kujitokeza kudhamini na wataona faida ya kile walichowekeza na kumuunga mkono Mhe: Rais kwa kukuza utamaduni wa Mtanzania.

No comments:

Post a Comment