Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11, 2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa; kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja; kubadilishana uzoefu; kuweka mikakati ya pamoja; na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari, uchumi wa buluu, na maendeleo endelevu ya uvuvi.
Aidha, Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.
No comments:
Post a Comment