Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewasili Wilayani Mafia, Mkoani Pwani kufanya ziara Maalum, leo tarehe 26 Oktoba, 2024.
Bashungwa amepokelewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Rashidi Mchatta, Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga na viongozi wengine wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
Katika ziara hiyo, Waziri Bashungwa atakagua huduma za usafiri wa vivuko, ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kilindoni, ataweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Raphta, ujenzi wa jengo la mama na mtoto (Maternity)pamoja na kuzungumza na wananchi.
No comments:
Post a Comment