DUWASA MTAA KWA MTAA MAHUNGU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 11, 2024

DUWASA MTAA KWA MTAA MAHUNGU


Katika kuhitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma ( DUWASA) imewatembelea wateja wake katika Mtaa wa Mahungu na kusikiliza changamoto walizonazo kuhusiana na hali ya huduma ya maji.

DUWASA imeahidi kutatua changamoto hiyo ndani ya kipindi kifupi kijacho cha miezi Mitatu kupitia Mradi wa Uchimbaji Visima Pembezoni unaoendelea.

Timu ya DUWASA imeongozwa na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Bi. Lena Mwakisale akiambatana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Bi. Rahel Muhando na Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Bw. Eliud Kitime.

DUWASA imetumia kikamilifu Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Oktoba 07 hadi kuhitimishwa Leo Oktoba 11, 2024 kwa kuwafikia wateja wake lengo likiwa ni kusikiliza changamoto zao na kuzitatua.

No comments:

Post a Comment