KAIMU KATIBU MKUU UTUMISHI AVUTIWA NA UBUNIFU WA UTOAJI MAFUNZO KWA WATUMISHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, October 28, 2024

KAIMU KATIBU MKUU UTUMISHI AVUTIWA NA UBUNIFU WA UTOAJI MAFUNZO KWA WATUMISHI


Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi akizungumza na watumishi wa ofisi yake wakati wa mafunzo yaliyolenga kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi na Watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Nyasinde Mukono akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) kuzungumza na watumishi kabla ya kuanza mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Wakurugenzi wasaidizi na watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Afisa Tehama Mkuu, Bi. Zalika Hussein akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-office) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bi. Georgina Kalanje akiwasilisha hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akizungumza nao wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mtumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Shukrani Mshigati, akichangia hoja wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa ofisi hiyo, Bw. Xavier Daudi (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kwenye mafunzo yaliyohusu kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Waratibu wa mafunzo kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora wakifuatilia mafunzo yaliyohusu kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi (aliyesimama) akizungumza jambo na watumishi wa ofisi yake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi hao katika masuala ya utendaji kazi yaliyofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.


Na. Lusungu Helela na Veronica Mwafisi

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi amesema amevutiwa na ubunifu wa kipekee unaoendelea kufanywa na Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu kwa kuja na mkakati wa kutoa mafunzo elekezi ya pamoja kwa Watumishi wote wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa ofisi mtandao (e-Office)

Bw. Daudi ametoa kauli hiyo leo Jumatatu tarehe 28 Oktoba, 2024 wakati akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambapo amesema ujio wa mafunzo ya kujengeana uwezo ni muhimu ikizingatiwa kwa sasa matumizi ya mfumo wa Ofisi Mtandao katika Ofisi za Serikali ni jambo lisiloepukika

Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bi. Nyasinde Mukono amesema mafunzo hayo yatakuwa yakifanyika kila Jumatatu asubuhi lengo likiwa ni kuwajengea uwezo watumishi wote.

"Tumekuja na utaratibu huu wa kujumuika kwa pamoja ili kuhakikisha watumishi wote wanakuwa na uelewa wa pamoja wa matumizi sahihi ya mfumo wa ofisi mtandao,” amesema Bi. Mukono.

Mafunzo hayo yamehudhuriwa na Watumishi pamoja na Wakurugenzi wa ofisi hiyo ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo matumizi ya saini ya kidigitali, tahadhari za kiusalama katika matumizi ya mfumo wa ofisi mtandao pamoja na namna bora ya kushughulikia barua kwa njia ya mfumo wa ofisi mtandao

Mada hizo zilizowasilishwa ziliongozwa na Wataalamu wa kutoka ndani na nje ya Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora zikiongozwa na mwenyeji wao Afisa Tehama Mkuu, Bi. Zalika Hussein.

No comments:

Post a Comment