"MTAA KWA MTAA" DUWASA NA WATEJA WA UDOM NA NASHERA HOTEL - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 9, 2024

"MTAA KWA MTAA" DUWASA NA WATEJA WA UDOM NA NASHERA HOTEL



Na Okuly Julius Dodoma


Ikiwa ni siku ya tatu ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imeendelea kuwatembelea wateja wake kutoa elimu,kusikiliza kero na kuzitatua.

Leo Oktoba 09,2024 DUWASA imemtembelea Mteja wake mkubwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na wamekutana na Mkurugenzi wa Fedha Dkt. MWANJAA LYAZIO ambaye amewapongeza kwa huduma ya maji wanayoipatia UDOM kwa kuzingatia wingi wa watu wanaowahudumia.

Dkt. Mwanjaa amewashukuru pia DUWASA kwa kuwatambua UDOM kama mmoja wa wateja wanayelipa Bili kwa wakati.

"tunawashukuru sana DUWASA kwa huduma ya maji, mnajua vyema kwamba UDOM ina idadi kubwa ya watu ila wote wanapata huduma ya maji kwa hili tuwape pongezi na pia mnatuvumilia pindi tunapopata changamoto yeyote," ameeleza Dkt. Mwanjaa

Menaja Huduma kwa Wateja Bi. Pendo Mkali, akiongozana na Kaimu Meneja wa Ankara na Madeni Bi. Irene Tesha wamesema UDOM ni moja ya Taasisi inayolipa Bili kwa Wakati hivyo DUWASA inawapongeza na kuwashukuru na kutaka taasisi zingine kuiga mfano wa Chuo hicho.

Meneja Huduma kwa wateja DUWASA Bi. Pendo Mkali (kushoto) akimpatia Hati ya Pongezi Meneja wa NASHERA HOTEL Bi. Salhe Huwel (kulia) kwa kutambua moja ya wateja wakubwa wanaolipa Bili kwa wakati.


No comments:

Post a Comment