Hali ya huduma ya maji mjini Lindi imetangamaa baada ya siku tatu za upungufu (tarehe 27-30, Septemba, 2024), hali iliyosababishwa na visima kutosukuma kiasi cha maji toshelevu kutoka chanzo cha maji cha Ng’apa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Lindi (LUWASA) Mhandisi Juma Sudi ameainisha mashine za kusukuma maji baada ya marekebisho hivi sasa zipo sawa, na kufafanunua kuwa huduma ya maji haijapungua kwa siku 21 kama ilivyokuwa imeripotiwa awali na baadhi ya vyombo vya habari.
Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji mjini Lindi ni asilimia 89 na kazi inaendelea katika kuimarisha huduma hiyo kwa wananchi.
Pichani: Mkazi wa Mtandaa Juu akiendela kupata huduma ya majisafi katika makazi yake leo.
No comments:
Post a Comment