NAIBU WAZIRI WA VIWANDA AIPONGEZA MATI SUPER BRANDS LTD KWA ULIPAJI KODI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, October 23, 2024

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA AIPONGEZA MATI SUPER BRANDS LTD KWA ULIPAJI KODI.



Ferdinand Shayo ,Manyara .


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameipongeza kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited kwa kuwa miongoni mwa walipa kodi wakubwa wanaolipa kodi vizuri nchini pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana .

Akizungumza wakati akitembelea banda la kampuni hiyo katika ufunguzi wa Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2024 yaliyofanyika katika Viwanja vya Stendi ya Zamani mjini Babati Mkoani Manyara .Naibu Waziri wa Viwanda amesema kuwa kampuni hiyo imekua na mchango mkubwa na kusaidia jamii inayowazunguka kupitia shughuli mbali mbali wanazozifanya.

"Niwapongeze kwasababu mnatoa ajira na zaidi ni walipa kodi wakubwa sana ,pia niwapogeze kwa vile mnavyosaidia shughuli za kijamii " Anaeleza Naibu Waziri wa Viwanda.

Kwa upande wake Afisa Masoko kampuni ya Mati Super Brands Limited Gwandumi Mpoma amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuzalisha vinywaji vyenye ubora wa kitaifa na kimataifa pamoja na kutoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana.

Mpoma ameipongeza serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji wa viwanda nchini na biashara kwa ujumla.



No comments:

Post a Comment