TUSHIRIKIANE KUTOA ELIMU JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, October 18, 2024

TUSHIRIKIANE KUTOA ELIMU JUU YA MABADILIKO YA TABIA NCHI


Na. Asila Twaha, OR - TAMISEMI


Afisa Wanyama Pori Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi.Hawa Mwechaga ametoa wito kwa wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu juu ya masuala ya mabadiliko ya  tabia nchi nchini.

Amesema mabadiliko hayo  husababishwa na nguvu za asili na shughuli za kibinaadamu ambazo sio rafiki kwa mazingira kwasababu huchangia ongezeko la gesi joto.

Bi. Hawa amesema hayo  Septemba 17,  2024 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja na wadau wa mabadiliko ya tabia nchi nchini.

"Kikao hiki kina lengo la kujadili namna bora ya kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinashiriki kikamilifu katika masuala  ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo kujenga uwezo  ili ziweze kunufaika na fedha zinazotolewa na Mifuko ya Kimataifa inayohusu Mazingira 'amesisitiza Bi Hawa


Amesema kuwa suala la mazingira ni jambo la  msingi kwa maendeleo ya wananchiwetu na mifumo ya ikolojia  inapatikana katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ametoa wito ili kuongeza jitihada za pamoja katika kukabiliana na athari za mabadiliko hayo ambayo yanaathiri uchumi, mazingira afya na ustawi wa jamii.

Naye Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa  James Messo amesema pamoja na Halmashauri kutenga bajeti   za usimamizi mazingira lakini amewaomba wadau kuendelea kushirikiana.

No comments:

Post a Comment