UWT YALAANI KUCHOMWA KITENGE CHENYE PICHA YA RAIS SAMIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, October 1, 2024

UWT YALAANI KUCHOMWA KITENGE CHENYE PICHA YA RAIS SAMIA



Na Mwandishi Wetu, Dodoma




UMOJA wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wamelaani vikali kitendo cha wanawake wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( BAWACHA) kuchoma kitenge chenye picha ya Rais samia suluhu Hassan kwa madai kuwa ameshindwa kukamilisha mambo Malimbali ikiwemo kupunguza gharama za maisha.




Hatua hiyo imekuja baada ya wanawake hao (BAWACHA) kuchoma vitenge walivyodai kupewa na Rais kwenye kongamano la siku ya wanawake Duniani machi 8 ,2023 wakati walipomualika kama Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo la wanawake wa Chadema, jambo linalotazamwa na UWT kuwa ni kuishiwa sera.




Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 1,2024 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa UWT Taifa Marry Chatanda, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameeleza kuwa tukio hilo ni lakitoto ,upuuzi huku akiwataka (BAWACHA) kuibua sera zenye mashiko kwa jamiii.


" Kwanza niseme jambo la kitenge kilichochomwa ni kitenge kinachoashiria kishindo cha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020/2025, kitenge hicho kilitengenezwa na UWT Taifa ikiwa ni sare kwa ajili ya kongamano la kumpongeza Rais samia kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyofanyika machi 19 2023 ,


Na kuongeza kuwa "toleo la kwanza la kitenge hicho lilitolewa machi 13, 2023 hivyo ni uongo kusema kuwa Rais Samia ndio aliyewagawia vitenge hivyo kwani siku wanafanya baraza lao kitenge kilikuwa bado hakijatengenezwa bali wanachama wa BAWACHA walinunua kitenge hicho ikiwa ni sare kwaajili ya kongamano ya kumpongeza Rais samia na tuliwaalika na waliudhuria kwa wingi, "amefafanua Chatanda


Pamoja na hayo Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, "Hivyo kitendo cha wana BAWACHA kununua na kuudhuria kwa wingi kwenye kongamano letu kunaashiria kwamba Rais samia ametekeleza mengi na waliyoyaeleza kwenye baraza kuu la BAWACHA, Machi 8, 2023 na kwamba wasiishie kuchoma vitenge bali pia waeleze ukweli waliwezaji kufanya baraza hilo, "amesema Chatanda


Aidha amesema Rais samia amefanya mambo makubwa na mazuri kwa Taifa katika nyanja zote hivyo badala ya kuchoma kitenge ni vyema wakatumia muda huo kutangaza fursa zote za kiuchumi ambazo Rais amekuwa akizipigania.


UWT inaendelea kutoa wito kwa jamii kuhakikisha inaendelea kulinda haki na kupinga vitendo vyote vinavyoendelea kwenye jamii ili kuwa na usalama na haki.


No comments:

Post a Comment