Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent L. Bashungwa amenadi Wagombea wa CCM na kubainisha sababu ya Wananchi kuchagua viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi kwa kuwa ndio Chama Pekee kinachosimamia misingi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa Watanzania.
Bashungwa ameeleza hayo Wilayani Karagwe leo Novemba 26, 2027 wakati akifunga kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji pamoja na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara katika Kata za Nyakabanga na Kayanga.
Bashungwa amebainisha miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Kata ya Kayanga ikiwa ni pamoja na maboresho ya miundombinu ya kituo cha afya cha Kayanga, ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kayanga, ujenzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Jengo la Halmashauri, ujenzi wa stendi ya Mabasi ya Kayanga na kufunga taa barabarani.
Aidha, Bashungwa amemuelekeza Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Karagwe kufanya usanifu wa uwekaji wa taa katika Soko Kuu la Kayanga pamoja na ujenzi wa mitaro ya maji inayokatisha katika Soko la Kayanga.
No comments:
Post a Comment