Na Okuly Julius _Dodoma
Wafanyakazi wa Wizara ya Madini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kusaidia kuharakisha agenda ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia madini mkakati yanayopatikana nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo Novemba 28,2024 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, wakati akifungua mkutano Mkuu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
"sekta ya madini ni Jicho la Serikali na Madini mkakati tuliyonayo yanapaswa kuchochea maendeleo ya nchi hasa katika eneo la Nishati safi ya kupikia kwani Dunia kwa sasa inaitazama Tanzania kama mfano wa kuigwa katika eneo hilo,"
Dkt. Kiruswa amewataka pia watumishi hao kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kuachana na vitendo vinavyoweza kudhoofisha maendeleo ya Sekta ya madini ikiwemo kujiepusha na vitendo vya Rushwa
" Kuna baadhi yetu wanawacheleweshea huduma wananchi bila sababu zozote hasa katika eneo la leseni za uchimbaji huku mkijua fika kuwa mnapo chelewesha leseni mnaichelewesha pia nchi kupata maendeleo kwani inapoteza mapato na wananchi nao wanailalamikia Serikali kwa ajili tu ya mtu mmoja anayekwamisha mambo
Na kuongeza kuwa "niwasihi katika utendaji kazi wenu zingatieni maadili ya Utumishi wa Umma katika kuwahudumia wananchi ili kuchochea maendeleo ya nchi, " ameeleza Dkt. Kiruswa
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Madini Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa Serikali imewapa wajibu wa kufanya tafiti kwa kutumia taasisi ya GST ambapo mpaka sasa wameshafanya kwa asilimia 16 lengo likiwa ni kufikia asilimia 50 ifikapo 2030
No comments:
Post a Comment