Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Bi. Agness Meena amekielekeza Chuo cha Maji kusimamisha ujenzi unaofanywa na mkandarasi katika moja ya majengo ya chuo hicho jijini Dar es salaam.
Akiwa pamoja na menejimenti ya Wizara ya Maji na Chuo cha Maji pamoja na mkandarasi wa jengo hilo amesema suala la usalama kwa watumiaji ni jambo la msingi.
Kufuatia uamuzi huo, ameunda tume ya wataalam itakayotoa majibu ya kiufundi na hatua madhubuti za kuchukua.
No comments:
Post a Comment