MwanaFA awataka wananchi Muheza wawachague wagombea wa CCM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 22, 2024

MwanaFA awataka wananchi Muheza wawachague wagombea wa CCM



Na: Mwandishi Wetu, Muheza.


MBUNGE wa Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo mhe Hamisi Mwinjuma almaarufu MwanaFA, ameshiriki uzinduzi wa kampeni kwa wagombea wa CCM wilayani Muheza na kuwanadi baadhi ya wagombea wawili kwa nyakati tofauti na kuwaomba wananchi wawague wagombea wa CCM ambao watashirikiana nao kuleta maendeleo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni kumnadi mgombea wa CCM Nuru Haji anayegombea nafasi ya Mwenyekiti kitongoji cha Kwamkabala MwanaFA amesema wananchi wilayani Muheza wawachague wagombea wa CCM kwa kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ana lengo la dhati la kuwarahisishia maisha Watanzania tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.

Amesema wakati anaomba kura mwaka 2020 katika mtaa huo wa Kwamkabala, wananchi walimuamini na wakamchagua wakati hakuwahi kuwa hata mjumbe wa nyumba mbili lakini walimpa kura za kishindo.

"Ndugu zangu mnaweza kushangaa tumekuja kumnadi mgombea wa Mwenyekiti wa kitongoji, CCM haina jambo dogo, lakini tumekuja kuwakumbusha Kwamkabala Ile ya mwaka 2020 na ya sasa ni tofauti," alisema.

Mbunge alisema wakati akiingia madarakani Kwamkabala ilikuwa na vyumba vitatu vya madarasa vya shule ya msingi lakini sasa eneo hilo tayari kwa miaka minne wamejenga shule mbili za msingi zilizokamilika.

Alisema Kwamkabala hakukuwa na mradi wowote wa maji unaotambulika na wananchi walikuwa wakipata adha kubwa ya maji hasa akina mama lakini sasa fikra zilizopo za wakazi wengi ni kuingiza maji hayo katika nyumba zao.

Alisema serikali ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni 1.1 katika eneo hilo kuhakikisha wanapata maji na mradi huo ukamilike Ili wananchi wapate maji ya uhakika.

Alisema eneo hilo wamechonga barabara mpya zaidi ya kumi kwa lengo la kuufungua mtaa huo huku mradi wa TASAF ambao huko nyuma haukuwepo umeweza kuwanufaisha zaidi ya watu 150.

"Sasa ndugu zangu asiyeshukuru kwa yai hata jogoo hachinjiwi, haya yote serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na chama Cha Mapinduzi imeyafanga Ili kurahisha maisha ya watu wa Kwamkabala na ndiyo lengo ambalo Mheshimiwa Rais analifanya kwa miaka hii minne," alisema.

Aliwataka wananchi wamchague mgombea wa CCM ambaye ni mtu makini anayefahamika na wanajamii wote na
kamwe wasichague wagombea ambao hawatambuliki mahali wanapokaa lakini pia ofisi za vyama vyao havitambuliki.

Alipomnadi mgombea wa CCM kitongoji cha Majengo Seif Twenye, alisema wananchi wa Muheza hawana sababu ya kuacha kuwachagua wagombea wa CCM ambao serikali imetekeleza miradi mingi katika Kila mtaa, Kijiji na kitongoji hivyo wanayo sababu ya kurudisha fadhila kwa kuendelea kuwachagua tena.

Pia alimmadi mgombea Mwenyekiti wa mtaa wa Genge kata ya Genge wilayani Muheza Hadija Kibaya ambako pia alirudia kueleza kwamba wananchi warudishe fadhila kwa CCM kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amepeleka miradi mingi ya maendeleo wilayani humo.



No comments:

Post a Comment