NAIBU WAZIRI MAHUNDI AKAGUA MINARA YA MAWASILIANO KATIKA MKOA WA MOROGORO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 3, 2024

NAIBU WAZIRI MAHUNDI AKAGUA MINARA YA MAWASILIANO KATIKA MKOA WA MOROGORO




Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, amekagua minara miwili ya mawasiliano ya kampuni ya Tigo iliyojengwa Mkoani Morogoro kwa ruzuku ya Serikali kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Akikagua minara hiyo Novemba 2, 2024, Mhandisi Mahundi amewaomba wananchi kuwa walinzi wa miundombinu ya mawasiliano inayojengwa kwa gharama kubwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Aidha, amesema kuwa ifikapo mwezi Mei 2025 minara yote 758 inayoendelea na ujenzi nchi nzima itakuwa imewaka na mawasiliano yatakuwa yameimarishwa nchini na kusaidia kukua kwa uchumi wa kidijitali.






No comments:

Post a Comment