NAIBU WAZIRI SANGU ASHANGAZWA NA IDADI NDOGO YA WAOMBAJI AJIRA KATIKA MIKOA YA KIGOMA, LINDI, MTWARA NA KATAVI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 18, 2024

NAIBU WAZIRI SANGU ASHANGAZWA NA IDADI NDOGO YA WAOMBAJI AJIRA KATIKA MIKOA YA KIGOMA, LINDI, MTWARA NA KATAVI


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Jamila Yusuph kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Katavi wakati akiwasili kwa ajili ya kuzngumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Sehemu ya Watumishi wa Halamashauri ya Wilaya ya Mpanda wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua wakati akizungumza nao ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Baadhi ya Wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakizungumza mbele ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangua kabla ya kuanza kuzungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao

Na Lusungu Helela- Katavi


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameonesha kushangazwa na idadi ndogo ya waombaji wa nafasi za kazi kada ya afya waliokuwa wameomba katika Mikoa ya Kigoma, Katavi, Lindi na Mtwara huku Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma ikiwa na idadi kubwa ya waombaji ukilinganisha na uhitaji.

Hatua hii inakuja kufuatia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kuweka utaratibu wa kuomba ajira katika mkoa husika kulingana na uhitaji ambapo Mwezi Juni mwaka huu ilitangaza jumla ya nafasi za kazi 9483 za kada ya afya ambapo kila muombaji alilazimika kuomba ajira katika mkoa ambao atafanya kazi endapo atafanikiwa kupita kwenye usaili.

Amesema licha ya tatizo kubwa la ajira linalowakumba vijana wengi lakini bado waombaji hao wanataka kuanza kufanya kazi katika Majiji makubwa jambo ambalo ni gumu

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.

Akitolea mfano Mkoa wa Kigoma mahitaji halisi ya waliotakiwa kuajiriwa katika kada ya afya ilikuwa ni 400 lakini waombaji wa nafasi hizo walikuwa hawazidi 200 huku Mikoa ya Lindi, Mtwara na Katavi nako idadi ni ndogo ukilinganisha na uhitaji.

Kufuatia hatua hiyo Mhe.Sangu ametoa wito kwa wazazi kuwashawishi watoto wao kuomba ajira pindi zinapotangazwa katika mikoa hiyo kwani uwezekano wa kupata ni mkubwa ukilinganisha na mikoa kama vile Arusha na Dodoma ambako ushindani ni mkubwa.

Hata hivyo Mhe.Sangu amewaonya wale watakaoomba kazi katika mikoa hiyo halafu wakapangiwa, Serikali haitawavumilia endapo wataanza kuomba uhamisho kabla ya kufanya kazi kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu.

Vilevile Mhe.Sangu amesema mikoa hiyo haina tofauti na Mwanza, Dar es Salaam, Dodoma na Arusha kwani ina fursa za kiuchumi pamoja na miundombinu iliyoboreshwa huku akiwataka wenye uhitaji wa ajira kuchangamkia ajira zinapotangazwa kwenye mikoa hiyo.

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Bw. Abert Msovela amesema licha ya uwepo wa fursa za kiuchumi katika mkoa huo lakini bado idadi ya Watumishi wa Umma wanaotuma maombi ya kutaka kuhama ni mengi.

Ametumia fursa hiyo kuwaasa Watumishi kubadili kasumba hiyo kwani Mkoa wa Katavi kwa sasa ni Mkoa wa kutimiza ndoto za kila Mtumishi mwenye kutaka kujikwamua kiuchumi kutokana na uwepo wa fursa lukuki za kiuchumi ikiwemo ardhi yenye rutuba.

No comments:

Post a Comment