NAIBU WAZIRI SANGU AWANADI WAGOMBEA, ATAJA SABABU ZA KUICHAGUA CCM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 25, 2024

NAIBU WAZIRI SANGU AWANADI WAGOMBEA, ATAJA SABABU ZA KUICHAGUA CCM



Na Mwandishi Wetu - Rukwa


Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Deus Sangu amewahimiza wananchi wa Kata ya Zimba na Mtowisa kuchagua wagombea wa CCM ili kuendeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Jimbo hilo.

Mhe.Sangu ambaye pia ni Mbunge wa Kwela Mkoani Rukwa ametoa kauli hiyo leo Novemba 25 kwa nyakati tofauti katika Kata ya Zimba na Mtowisa zilizopo katika Jimbo hilo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kimkakati ya Kampeni zinazoendelea za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye Jimbo hilo .

Amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Jemedari Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetekeleza miradi ya lukuki ya maendeleo katika Jimbo la Kwela ambayo haijawahi kutokea tangu nchi hii ilipopata uhuru.

Ameitaja baadhi ya miradi hiyo inayotekelezwa ikiwemo ujenzi wa madaraja, vituo vya afya, elimu , maji pamoja na umeme.

Amesema CCM chini ya Uongozi madhubuti na wenye maono wa Ras Mhe.Samia Suluhu Hassan una nia ya kuendelea kuleta maendeleo katika Jimbo hilo huku akiwataka wananchi kuwachagua Wagombea wa CCM.

“Nawaomba msifanye kosa la kuwachagua vyama vingine maana wanataka vyeo tu, msikubali watu wanaowaambia mkunje ngumi hawana ilani iliyopitishwa na wananchi wala bajeti wanataka muwachague wakafanye kazi gani?,” amehoji Mhe.Sangu

Ameongeza kuwa " Vyama hivyo havina Serikali na vinaenda kufanya nini kama vitachaguliwa hivyo acheni kupoteza muda hapa wagombea sahihi ni CCM pekee" amehoji Mhe.Sangu




No comments:

Post a Comment