SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO IMEPUNGUZA UHALIFU WA MTANDAO- ACP MWANGASA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 19, 2024

SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO IMEPUNGUZA UHALIFU WA MTANDAO- ACP MWANGASA


Na mwandishi wetu


ACP Joshua Mwangasa, Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Tanzania amesema kuwa kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 kesi nyingi zilizokuwa zikiripotiwa zilikuwa hazifiki mwisho kwasababu ya kukosekana kwa vifungu vinavyohusisha makosa ya mtandao moja kwa moja kutoka kwenye sheria ya msingi ya Penal Code.


Amesema kuwa utungwaji wa sheria hiyo umekuwa na mafanikio makubwa kwa kupunguza makosa ya uhalifu wa mtandao kwa wananchi kuripoti matukio ya uhalifu wa mtandao katika vituo vya polisi na kushughulikiwa ipasavyo.

Ameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi Tanzania, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wananchi na wadau wengine katika utoaji wa elimu kwa umma na ushughulikiaji wa makosa hayo.

No comments:

Post a Comment