TANZANIA KUANDAA WORLD TRAVEL AWARDS 2025 KWA BARA LA AFRIKA – DKT ABBASI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 26, 2024

TANZANIA KUANDAA WORLD TRAVEL AWARDS 2025 KWA BARA LA AFRIKA – DKT ABBASI

 


Na John Mapepele 

Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi amesema Tanzania inakwenda kuandaa Tuzo za Utalii duniani (World Travel Awards, WTA) kwa Bara  la Afrika  kwa mwaka 2025.

Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo Novemba 26, 2024 wakati akiongea na Vyombo vya Habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kutoka nchini Ureno  ambapo Tanzania  ilitwaa  Tuzo ya Dunia  ya Sehemu Maridhawa Zaidi kwa Utalii wa Safari 2024 (World’s Leading Safari Destination) usiku wa kuamkia jana.

Dkt. Abbasi amefafanua kuwa Tanzania imepata Tuzo hiyo kutokana na ushirikiano mkubwa wa wadau mbalimbali wa Utalii nchini katika  kutangaza   vivutio vya utalii.

Aidha, amesema kazi kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza Tanzania kupitia Filamu ya The Royal Tour na Amazing Tanzania imesaidia kuitangaza Tanzania kimataifa.

Ameongeza  kuwa  Tuzo hizo ni ishara  ya  kwamba  wageni wamekuwa na imani kubwa  na vivutio vya utalii  na ukarimu ambao wamekuwa wakipata  wakati  wanapokuja kutembelea vivutio hivyo na kuwataka  kuendelea kuwa wakarimu.

Ametoa wito  kwa watanzania  wote  kushirikiana na Serikali katika kulinda na kuhifadhi  vivutio vya utalii na raslimali zilizopo ili viweze  kuchangia kwenye   uchumi wa taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru amesisitiza kuwa kwa sasa  Tanzania inakwenda  kutangaza mazao  mapya ya utalii ili kupanua wigo wa  vivutio vya utalii  na hivyo kuwafanya wageni kuongeza siku za kukaa  na kutumia wakifika nchini.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt. Thereza Mugobi amesisitiza  wadau wote nchini kuzingatia  sera na kanuni mbalimbali zilizowekwa na Serikali ili  sekta ya utalii nchini iendelee kukua.

No comments:

Post a Comment