UCHIMBAJI VISIMA MAENEO YA PEMBEZONI KUPUNGUZA ADHA YA MAJI DODOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 20, 2024

UCHIMBAJI VISIMA MAENEO YA PEMBEZONI KUPUNGUZA ADHA YA MAJI DODOMA




NA,Mwandishi Wetu, DODOMA


MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imesema ili kupunguza adha ya upatikanaji wa huduma ya maji na mgao kwa wananchi inaendelea kuchimba visima maeneo ya pembezoni ikiwemo mradi wa Nzuguni ambapo zaidi ya sh. bilioni 4.3 zimetumika.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph mara baada ya wajumbe Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) kufanya ziara ya kutembelea maeneo ya miradi inayotekelezwa ili kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika jiji la Dodoma.

Alisema mahitaji ya maji kwa jiji la Dodoma ni lita milioni 149 lakini uzalishaji ni lita milioni 52 hivyo kufanya kuwa na upungufu ambao umesababisha huduma hiyo kutolewa kwa migao.

Alitaja miradi mingine inayotekelezwa kuwa ni Nala ambapo unagharimu sh.bilioni 1.5 kwa awamu ya kwanza ambao umefikia asilimia 80 na muda sio mrefu utaanza kutoa huduma kwa wananchi.

“Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya muda mfupi na mrefu lengo ni kuhakikisha inapunguza adha ya upatikanaji maji Dodoma.Tuna mradi wa Ihumwa, Njedengwa ambao umegharimu sh.bilioni 2.7 na umekamilika kwa asilimia 100 na tayari umeanza kutoa huduma kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Mhandisi Aron alisema DUWASA inaendelea kutekeleza mradi wa nzuguni awamu ya pili ambapo hivi sasa upo katika hatua za manunuzi na mradi huo unatarajia kuzalisha maji mengi kuliko mradi wa awamu ya kwanza.

Alisema mradi huo ukikamilika utaondoa mgao wa maji kwa wananchi wa Meriwa,Ilazo,Ipagala,Area C na D

“Tunaendelea na ujenzi wa bwawa la farkwa fedha za kupata ujenzi wa awamu ya kwanza zimeshapatikana lengo letu ni kuhaakikisha ifikapo machi mwakani mkandarasi awe eneo la mradi akiendelea na kazi,”alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji Maji DUWASA Bernard Rugayi alisema hali ya uzalishaji maji Dodoma ni asilimi 52.

Alisema uzalishaji huo haukidhi mahitaji, serikali inaendelea na jitihada mbalimbali za kutafuta vyanzo mbalimbali vya maji ili kuhakikisha huduma hiyo muhimu inaendelea kuimarika.

“Serikali inatekeleza miradi wa maji Nzuguni ambapo kwa awamu ya kwanza umekamilika kwa asilimia 98 huku utekelezaji wa awamu ya pili ukiendelea ili uweze kuwanusfaisha watu wengi zaidi,”alisema

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la EWURA CCC, Stella Lupimo alisema wameridhishwa na namna DUWASA inavyotekeleza majukumu yake na mipango iliyopo ya kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi na usafi wa mazingira Dodoma.

Alisema Dodoma inakuwa kwa kasi na mahitaji yam aji yanakuwa hivyo ni matumaini ya Baraza kuwa katika mipango ya DUWASA itaangalia takwimu za ukuaji wa watu.

“Tunatoa wito kwa watumiaji wa huduma za maji ambazo zinatolewa na DUWASA kuhakikisha wanaendelea kutunza miundombinu ya maji,”alisema


No comments:

Post a Comment