UPANDIKIZAJI INI MUHIMBILI SASA NI 2025 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 24, 2024

UPANDIKIZAJI INI MUHIMBILI SASA NI 2025



Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeanza matayarisho kuelekea upandikizaji wa ini, ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa azima ya Serikali ya kutoa huduma za ubingwa bobezi nchini, ili kusogeza huduma hizo karibu na wananchi ambazo hazikuwepo kutokana na utalaam, vifaa vya uchunguzi au miundombinu stahiki ya kutolea huduma hizo hivyo kuigharimu fedha nyingi kupeleka wagonjwa hao kutibiwa nje ya nchi.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi amesema, hospitali imeingia makubaliano na Hospitali mbalimbali duniani zenye ujuzi huo ili kuanza matayarisho kwa kushirikiana na watalam wazalendo kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwaka 2025, Tanzania inaanza kutoa huduma hiyo kwani miundombinu stahiki ipo na vifaa tiba vya uchunguzi.

“Wiki hii tumeshirikiana na watalaam kutoka Hospitali ya Fortis ya nchini India ambao wamekua na madaktari wetu ambapo kwa siku tatu wameona wagonjwa zaidi ya 100 wenye changamoto mbalimbali za magonjwa ya ini na kuthamini hali ya upatikanaji wa dawa, miundombinu ya maabara, ICU ambayo inakidhi mahitaji ya huduma hiyo”, amesisitiza Prof. Janabi.

Kwa upande wake bingwa mbobezi wa upandikizaji ini Dkt. Gaurav Gupta kutoka Hospitali ya Fortis na Bi. Jenifer Choudhary, Mkurugenzi wa Biashara kutoka Vaidam Health wamesisitiza kuwa watatoa ushirikiano na utalaam unaohitajika kuhakikisha MNH inafikia lengo la uanzishwaji wa huduma hii hapa nchini.

Naye Bingwa Mbobezi wa Upasuaji wa Magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini na Bingwa wa Upasuaji kupitia Tundu Dogo, Dkt. Kitembo Salumu amesema, mpaka sasa takwimu za Hospitali zinaonesha kuwa kuna zaidi ya wagonjwa 5,000 wenye shida kwenye ini ambapo kati yao 2,333 wana uvimbe kwenye ini na 607 wamegungulika kuwa na tatizo la saratani ya ini, wengine maini yamesinyaa hivyo wote wanahitaji huduma ya kupandikizwa ini.


No comments:

Post a Comment