Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu leo Novemba 17, 2024 ameungana na Mawaziri wa kisekta wanaoshughulikia masuala ya Maafa katika zoezi la uokoaji wa watu walionasa kwenye jengo lililoporomoka Kariakoo kwenye Mtaa wa Congo na Mchikichi Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Viongozi wengine waliofika katika eneo hilo ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Thobias Makoba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum Bw. Amon Mpanju pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Anderson Mutatembwa katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment