WAKANDARASI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA KWENYE MIRADI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, November 5, 2024

WAKANDARASI WATAKIWA KUZINGATIA UBORA KWENYE MIRADI




Na Okuly Julius Dodoma


Serikali imewataka Wakandarasi wanaopewa Dhamana ya kutekeleza miradi ya maji kuhakikisha wanazingatia ubora Kulingana na matakwa ya Mikataba yao.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew baada ya kushuhudia utiaji saini wa Ujenzi wa Mradi wa Maji wa Handali Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma wenye thamani ya shilingi milioni 609 unaotekelezwa na RUWASA kupitia Mkandarasi JISHAM AND CONSTRUCTION COMPANY LIMITED

"kisima cha Kwanza Tanzania kilichimbwa Dodoma mwaka 1931 Makutopora, sambamba na vile ambacho vilivyochimbwa mwaka 1963, 1967,1970 na mpaka leo bado vinafanya kazi vizuri Sana kwa sababu vilizingatia ubora na thamani ya pesa iliyokuwa imetumika,"

Na kuongeza '' Wito wangu kwa Wakandarasi baada ya kutia saini katika mradi huu ni kuona ubora ukizingatiwa na matumizi sahihi ya vifaa vinavyotakiwa vitumike ili wananchi hawa wapate maji ya uhakika na salama kwani hakuna sababu yeyote wala kikwazo cha kujenga chini ya kiwango, "amesisitiza Mhandisi Kundo

Pia Mhandisi Kundo amesema katika mradi huo kuna kilometa 14.58 za mtandao wa bomba hivyo kumwelekeza mkandarasi kuhakikisha bomba hizo zinakuwa imara ili kuepusha kupasuka kutokana na presha ya maji kwani lengo la serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Maji ni kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na wananchi wapate huduma ya Kudumu ya maji.

Pia amewataka RUWASA kuhakikisha mtandao wa Mabomba unaokwenda katika Magati au DP 16 zote zilizoanishwa katika mradi huo zinatoa maji na isitokee hata moja kutotoa maji kwa sababu zozote ile.

"waambieni wananchi ukweli kama DP zipo 16 zitoe maji zote kwani hatuwezi kuvumilia kuona DP 4 tu kati ya hizo zote ndio zinatoa maji ni bora kujenga 4 na zitoe maji ya uhakika," ameeleza Mhandisi Kundo

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mhe. Livingstone Lusinde ameishukuru serikali kwa miradi ya maji iliyopo na inayoendelea kujengwa katika jimbo lake kwani kuna vijiji ambavyo havijawahi kupata maji tangu uhuru ila sasa wanapata maji safi na salama.

"naishukuru Serikali kwa ujenzi wa mradi wa kuchuja maji yenye chumvi pale Ndogoye ila sasa niwaombe pia kuwakumbuka watu wa Kata ya Manzase kwani maji ya pale unaweza kupikia mboga bila Chumvi hivyo mradi wa Ndogoye ukifanikiwa tunaomba napo tupakumbuke ili wapate maji safi na salama Yasiyokuwa na Chumvi.

Nao baadhi ya wananchi wamemshukuru Mbuge wao kwa kuendelea kuwawakilisha vyema na kupeleka hoja zao Serikalini na matokeo yake wanapata miradi mbalimbali ikiwemo Maji, umeme, na Shule.







No comments:

Post a Comment