WITO WATOLEWA KWA JAMII KUISOMA NA KUIJUA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 22, 2024

WITO WATOLEWA KWA JAMII KUISOMA NA KUIJUA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015


Wakili wa Serikali Mwandamizi, Bw. Ramadhani Jongo kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ametoa wito kwa jamii kuisoma na kuijua Sheria ya ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 ambayo inapatikana katika tovuti ya Wizara hiyo (www.mawasiliano.go.tz) na tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (www.tcra.go.tz) kwa lengo la kufahamu haki na wajibu wao katika sheria hiyo.

Wito huo umetolewa leo Novemba 22, 2024 katika ofisi za Wizara hiyo jijini Dodoma alipokuwa akizungumzia masuala ya matumizi salama ya mtandao.

Ameongeza kuwa, sheria hiyo inaelezea bayana makosa ya mtandao ni yapi na adhabu zake ni zipi hivyo jamii inapaswa kuifahamu vizuri sheria hiyo ili kuwa na uelewa mpana wa haki zao na wajibu wao, kwani kutokujua sheria hakumuondolei mtu hatia pale anapovunja sheria.

Imeandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

No comments:

Post a Comment