OSHA YAGUSA MAISHA YA WAKAZI WA MKOA WA KILIMANJARO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 10, 2026

OSHA YAGUSA MAISHA YA WAKAZI WA MKOA WA KILIMANJARO

Mgeni Rasmi wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka, akiwahutubia washirikiwa bonanza.

******************

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umegusa maisha ya wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kupitia kampeni yake ya huduma kwa jamii ambapo imekabidhi vifaa vya msaada katika mashule, hospitali pamoja na kutoa mafunzo ya usalama na afya kwa wajasiriamali wadogo zaidi ya 500.

Makundi yaliyonufaika na kampeni hiyo ni kutoka Wilaya za Mwanga na Moshi Mjini ambapo OSHA imepanda miti 200 ya matunda katika shule mbalimbali za msingi na sekondari ndani ya Wilaya ya Mwanga.

Aidha, imekabidhi mashuka 100 katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga, vifaa vya michezo pamoja na kutoa mafunzo ya usalama na afya yaliyofanyika sambamba na kukabidhi vifaa kinga kwa makundi ya wajasiriamali wadogo wenye ulemavu pamoja na maafisa usafirishaji (bodaboda).

Akizungumza katika kilele cha kampeni hiyo katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi, Mgeni Rasmi wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka, amesema lengo la kampeni hiyo ni kugusa maisha ya makundi yenye mahitaji maalum katika jamii.

“Miongoni mwa makundi yaliyonufaika na kampeni hii ni pamoja na Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) 200 wa Wilaya ya Mwanga na Moshi, Wanachama 70 kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA), Shule za Sekondari Mwanga pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mwanga.”

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, amesema tukio hilo ni utekelezaji wa mkakati wa OSHA wa kurudisha kwa jamii sambamba na utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kusimamia uzingatiaji wa kanuni bora za usalama na afya katika maeneo ya kazi nchini.

“Jukumu letu kubwa ni kuhakikisha maeneo ya kazi yanakuwa na mifumo madhubuti yakuwalinda wafanyakazi dhidi ya vihatarishi vya ajali, magonjwa na vifo mahali pa kazi. Sambamba na utekelezaji wa majukumu yetu, tumekuwa na desturi ya kuwa na shughuli zinazogusa maisha ya watu katika kipindi ambacho tunashiriki mashindano yaSHIMIWI,” ameeleza Kiongozi Mkuu wa OSHA.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga Mpampalika Mfaume pamoja na wanufaika wa kampeni hiyo, wameishukuru Taasisi ya OSHA kwa kubana matumizi yake ili kuwezesha upatikanaji wa mahitaji ya msingi kwa makundi mbalimbali ya jamii.

“Nimefurahia mafunzo ya leo kwasababu nimefahamu kazi za OSHA na zaidinimejifunza kwamba usalama si tu kwa wafanyakazi walioajiriwa bali hata kwetu sisituliojiajiri tunatakiwa kuzingatia kanuni bora za usalama na afya kwa ajili ya usalama wetu wenyewe,” ameeleza Bi. Judika Allen Mshiriki wa Mafunzo.

Kampeni hiyo ya OSHA ya huduma kwa jamii ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka kama sehemu ya ushiriki wa Taasisi katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara, Idara na Wakala za Serikali (SHIMIWI), imehitimishwa kwa Bonanza OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Polisi Moshi Oktoba 08, 2026.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akitoa salamu za ukaribisho katika Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyikaViwanja vya Shule ya Polisi Moshi Oktoba 8, 2026.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akifuatilia matukio katika Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika Viwanja vya Shule ya Polisi Moshi Oktoba 8, 2026.
Mgeni Rasmi wa Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka akiwa na Mtendaji Mkuuwa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, katika Bonanza la OSHA la Huduma kwa Jamii (OSHA CSR Bonanza 2026) lililofanyika Viwanja vya Shule ya Polisi Moshi Oktoba 8, 2026.
Maafisa usafirishaji (bodaboda) waliopatiwa mafunzo ya usalama na afya na OSHA katika kampeni ya huduma kwa jamii iliyotekelezwa na OSHA katika Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 7-8, 2026 wakikabidhiwa vifaa kinga na Mgeni Rasmi wa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, akipanda mti katika Shule ya Sekondari Vudoi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya huduma kwa jamii iliyotekelezwa na Taasisi yakekatika Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 7-8, 2026.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga Mpampalika Mfaume na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hospitali ya Wilaya ya Mwanga mara baada ya OSHA kukabidhi msaada wa mashuka 100 katika hospitali hiyo.
Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, Katibu Tawala wa Wilaya ya Mwanga Mpampalika Mfaume na viongozi wengine wa Wilaya ya Mwanga wakionesha mashuka yaliyokabidhiwa na OSHA katika Hospitali ya Wilaya ya Mwanga.
Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza, Moteswa Meda, akitoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri ya Mwanga pamoja na Maafisa usafirishaji ikiwa ni sehemu ya kampeni yaOSHA ya huduma kwa jamii iliyofanyika Mkoani Kilimanjaro tarehe 7-8, Oktoba, 2026.
Baadhi ya maafisa usafirishaji (bodaboda) waliopatiwa mafunzo ya usalama na afya na OSHA katika kampeni ya huduma kwa jamii iliyotekelezwa na OSHA katika Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 7-8, 2026 wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa vifaa kinga na Mgeni Rasmi wa tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka.

No comments:

Post a Comment