DUWASA YAIPA MATUMAINI DODOMA, MAJITAKA YA MTUMBA KUTIBIWA NA KUTUMIKA KWENYE KILIMO CHA UMWAGILIAJI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, October 10, 2026

DUWASA YAIPA MATUMAINI DODOMA, MAJITAKA YA MTUMBA KUTIBIWA NA KUTUMIKA KWENYE KILIMO CHA UMWAGILIAJI.


Na Erick Nenda, OKULY BLOG - DODOMA


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ukusanyaji na uchakataji wa majitaka kutoka Mji wa Serikali  Mtumba unaolenga kuboresha usafi wa mazingira na kuwezesha maji yatakayochakatwa kutumika kwa umwagiliaji baada ya kuthibitishwa kuwa yanafaa kwa matumizi hayo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo Rais wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Annastazia Rugaba na wanachama wa PRST baada ya kukamilika kwa mkutano wao mkuu wa mwaka (AGM) amesema uwekezaji huo unaonesha umuhimu wa kupanga miundombinu ya mazingira sambamba na ujenzi wa miji mipya ili kuzuia changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye.

Mradi huo umeelezwa kuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha miundombinu ya maji na majitaka katika mji wa Serikali, pia ameipongeza DUWASA kwa kuzingatia mifumo ya majitaka katika mipango ya maendeleo ya mji huo.

“Tunaposema masuala ya environmental sustainability na governance ni mambo kama haya,wakati tunaujenga mji wetu wa Mtumba mji wa Serikali tunaangalia pia mifumo ya majitaka itakuwaje,” amesema Rugaba.

Amesema amefurahishwa na maelezo ya kitaalamu kuhusu namna mfumo huo utakavyokusanya majitaka kutoka Mji wa Serikali na kuyapeleka katika eneo maalumu kwa ajili ya kuchakatwa mradi huo pia unatoa fursa ya kujifunza kwa wataalamu wa ndani na kuongeza uwezo wa Watanzania kusimamia miradi mikubwa ya miundombinu.

Kwa upande wake, Mhandisi mkazi wa miradi ya DUWASA, Severine Mkenda amesema kazi zinazotekelezwa zinahusisha miradi ya maji safi usambazaji wa maji katika Mji wa Serikali na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha majitaka kwenda eneo la uchakataji ameeleza kuwa mtandao wa mabomba ya majitaka kutoka Mji wa Serikali unatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 40 huku bomba la kuyasafirisha hadi eneo la uchakataji likiwa na urefu wa kilomita 15.

Amesema ujenzi wa mabwawa ya uchakataji ulikuwa umefikia takribani asilimia 50 wakati wa maelezo yake huku mkandarasi akipanga kuongeza kasi ya kazi ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua nyingi.

“Mkandarasi hapa amejipanga kufanya kazi usiku na mchana ili kama El Nino ikitokea tuwe tumekamilisha kazi kubwa ya ujenzi wa mabwawa haya angalau kwa asilimia 90 hadi 95,” amesema mkenda.

Aidha mradi huo unatarajiwa kunufaisha pia wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka eneo la uchakataji kwa kuwa maji yatakayopitia katika mfumo huo yanaweza kutoa fursa ya kuendeleza kilimo cha mboga na shughuli nyingine za umwagiliaji zitakazoruhusiwa kulingana na viwango vya ubora wa maji hata ivyo maabara inajengwa kwa ajili ya kupima ubora wa maji mara kwa mara ili kuhakikisha matumizi yake hayahatarishi afya za wananchi.

Mradi wa majitaka wa Mtumba unaweka msisitizo katika umuhimu wa kuunganisha maendeleo ya miji usimamizi wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali za maji Kukamilika kwa mradi huo pamoja na kuhakikisha maji yaliyosafishwa yanapimwa na kuthibitishwa kuwa salama kwa matumizi.

No comments:

Post a Comment