Na Okuly Julius _Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga amesema ili kukabiliana na Ugonjwa wa UKIMWI jitihada zakumfikia na kumshirikisha kila anayeishi na Virusi vya Ukimwi (VVU) aliyepata madhara ya UKIMWI na walio katika hatari ya kuambukizwa.
Nderiananga ameyasema hayo leo Novemba 14,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi habari kuelekea maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yenye kauli mbiu: "Chagua njia sahihi, Tokomeza Ukimwi" ambapo amesema bado kumekuwa na kuongezeka kwa ushamiri miongoni mwa baadhi ya makundi yakiwemo vijana kati ya umri 15-24 , madereva wa masafa marefu, wachimbaji wadogo wa madini na wavuvi.
"Ili kumaliza UKIMWI tunapaswa kumfikia na kumshirikisha kila anayeishi na VVU, aliyepata madhara ya UKIMWI na walio katika hatari ya kuambukizwa VVU,"
Na kuongeza kuwa "Usawa wa Kijinsia umefungamanishwa na haki za binadamu ambacho ni kipengele muhimu sana kwenye mwitikio wa UKIMWI. Aidha, kukubalika, kuthaminiwa na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU vinachangia kuimarisha afya zao. Kutokana na hilo, ubaguzi na unyanyapaa kwa sababu zozote zile ni kikwazo kwenye kupata huduma za kinga dhidi ya VVU, upimaji wa hiari, tiba na matunzo, "ameeleza Nderiananga
Aidha amesema matokeo ya utafiti wa viashiria vya UKIMWI wa mwaka 2022/2023 idadi ya watu wanaoishi na VVU nchini inakadiriwa kuwa 1,540, 000 ukilinganisha na takriban watu 1,700,000 mwaka 2016/17 na ushamiri wa Virusi Vya UKIMWI ( VVU) kitaifa ni asilimia 4.4 ikilinganishwa na asilimia 4.7 kwa mwaka 2016/17.
Ametoa wito kwa wanajamii na wadau wote kushirikiana katika kupanga na kutekeleza shughuli za kudhibiti VVU na UKIMWI kwa kuzingatia vipaumbele na mahitaji ya mahali walipo. Katika utekelezaji wa hilo, usawa hasa wa kijinsia na katika utoaji huduma kwa misingi ya haki ni nguzo kubwa katika kutimiza ndoto yetu ya kumaliza VVU na UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa TACAIDS Dakta Jerome Kamwela amewataka wanaotumia Dawa za kufubaza Virusu vya UKIMWI kuhakikisha wanatumia dawa hizo kama wanavyoelekezwa na wataalamu wa Afya
MATUKIO KUELEKEA KILELE CHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI
Tarehe 22/11/2024 wadau watagawiwa mabanda ya Maonyesho. Naomba kuchukua fursa hii kuhimiza wadau wote kuwahi ili wapate muda wa kuandaa shughuli zao na kuwa tayari kwa ajili ya maonyesho na utoaji huduma;
Tarehe 24/11/2024 kutakuwa na Ufunguzi rasmi wa wiki ya maadhimisho ambao utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwenye Uwanja wa Mpira wa Maji Maji;
Tarehe 25 - 26 /11/2024 Tumepanga kufanya mdahalo wa Vijana na Viongozi wa Kidini na Kimila ambapo Waziri wa Afya Mheshimiwa Jenista Mhagama atakuwa mgeni rasmi. Midahalo hii itafanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa Parokia ya Bombambili;
Mnamo tarehe 29 - 30/11/2024 kutakuwa na Kongamano la Kitaifa la Kisayansi kwa ajili ya kujadili mada mbalimbali kuhusu mwitikio wa taifa wa UKIMWI. Kongamano hili litafunguliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge, Mhe. William Lukuvi katika ukumbi Chidamali;
Tarehe 30/11/2024 kutakuwa na kilele cha Matukio ya Vijana. Tukio hili ni hitimisho la huduma rafiki ambazo zitakuwa zinatolewa tangu ufunguzi wa maadhimisho kwenye Uwanja wa Mpira wa Maji Maji. Mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge; na
Tarehe 01/12/2024 ndio Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kitaifa ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Phillip Isdor Mpango atakuwa Mgeni Rasmi.
Maadhimisho hayo yanafanyika kila mwaka Disemba mosi, ambapo mwaka huu Kitaifa yatafanyika Mkoani Ruvuma na Mgeni rasmi anatarajia kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.

No comments:
Post a Comment