Dkt. Abbasi Ahimiza Utalii wa Ndani Pori la Akiba Pande Dar - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 9, 2024

Dkt. Abbasi Ahimiza Utalii wa Ndani Pori la Akiba Pande Dar


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Desemba 9, 2024 amesherehekea miaka 63 ya Uhuru kwa kutembelea Pori la Akiba la Pande lililopo nje kidogo ya jijini la Dar es salaam na kuzungumza na menejimenti pamoja na wafanyakazi akihimiza kuvutia watalii zaidi wa ndani lakini nje pia.

Akizungumza na menejimenti ya Pori hilo, Dkt. Abbasi ameelekeza kuboreshwa kwa pori hilo ikiwemo kuongeza wanyama zaidi ili wananchi wa Dar es salaam na mikoa ya karibu waweze kutalii katika eneo hilo.

Amesisitiza pia watumishi kuzingatia maadili katika kazi zao na kufanya kazi kwa bidiii ili kuendeleza pori hilo ili liweze kuongeza idadi ya watalii wa ndani.

Pori la Akiba la Pande linakupatia fursa ya kufanya utalii wa Bustani ya Wanyamapori Hai kama Simba, Chui, Nyumbu, Pundamilia, Swala na Ndege aina mbalimbali lakini na maeneo ya kambi maalum, sherehe mbalimbali na matembezi ya msituni ili kujenga afya.






No comments:

Post a Comment