MAT BULDERS WEKEZENI DODOMA, KASEKENYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 2, 2024

MAT BULDERS WEKEZENI DODOMA, KASEKENYA



Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amesema Mkoa wa Dodoma una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya ujenzi wa teknolojia ya kisasa
na sekta nyingine.

Amesema hayo, wakati akifunga maonesho Maalum ya Mat Builders Miners and Contractors Global Expo yaliyofanyika kwa siku 10 jijini Dodoma.

"Mji wa Dodoma ndio makao makuu ya nchi na unakua kwa kasi hivyo unahitaji uwekezaji mkubwa wa teknolojia ya kisasa ya ujenzi" amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Aidha, amesema Serikali inaweza kuongeza kasi ya uwekezaji kupitia ujenzi wenye tija na wa kisasa kwa kushirikisha wadau mbalimbali katika sekta ya ujenzi na nyingine na kuzisimamia kitaifa na kimataifa kupitia maonesho ya Mat Builder global Expo.

Maonesho hayo yalioandaliwa na kampuni ya Ujenzi ya Mat Builder yameshirikisha Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi,washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na wajasiriamali lengo likiwa kuonesha na kuhamasisha teknolojia ya kisasa katika sekta ya ujenzi.

Maonesho hayo yameongozwa na kauli mbiu kauli mbiu isemayo "mwendelezo wa sekta ya ujenzi kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa kwa uweledi kimataifa".

Zaidi ya taasisi tano na wataalam wa masuala ya ujenzi wameshiriki maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment