MTOTO ALIYEZALIWA KABLA YA MUDA, MAMA YAKE ALIFARIKI AKABIDHIWA KWA NDUGU ZAKE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, December 29, 2024

MTOTO ALIYEZALIWA KABLA YA MUDA, MAMA YAKE ALIFARIKI AKABIDHIWA KWA NDUGU ZAKE



Na Jeremiah Mbwambo, Dodoma


Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Benjamin Mkapa Mwanaidi Makao amemkabidhi mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati na ikiwa mama mzazi wa mtoto huyo amefariki.

"Nawapongeza wauguzi na madaktari kwa namna walivyo muhudumia mtoto huyu kama tunavyo fahamu mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati anahitaji joto kutoka kwa mzazi wake kwa kuwa mtoto huyu alifiwa na mama yake huko alipokuwa akipatiwa huduma za uzazi hivyo walimleta hapa kwetu ili kuokoa maisha yake hivyo wauguzi walikuwa wakimuhudumia kama mzazi" Amesema Mwanaidi

Ameongeza kuwa kwa sasa mtoto huyu anaruhusiwa akiwa na afya nzuri

"Bibi tunakukabidhi mtoto huyu tunakuomba mumtunze na aendelee kuwa na afya njema zaidi ya alivyo sasa" amesema Mwanaidi

Kwaupande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto Julieth Kabengula ametoa shukrani zake kwa serikali na uongozi wa Hospitali

"Namshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwekea vifaa vya kisasa ambavyo vimetufanya tuokoe maisha ya watoto, kipekee nimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kuridhia matumizi mbalimbali kwaajili ya kuokoa maisha ya huyu mtoto, mtoto aliletwa akiwa na uzito chini ya kilo moja sasa tunamruhusu akiwa na kilo 1.9" amesema Dkt. Kabengula

Hospitali ya Benjamin Mkapa imekuwa ikiwahudumia watoto walio zaliwa kabla ya wakati kwa mafanikio makubwa.

No comments:

Post a Comment