PROF. KUSILUKA: VYUO VIKUU VIWEKE MKAZO KWENYE MAFUNZO YA AKILI MNEMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 4, 2024

PROF. KUSILUKA: VYUO VIKUU VIWEKE MKAZO KWENYE MAFUNZO YA AKILI MNEMBA




Na Okuly Julius _ Dodoma


Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) PROF LUGANO KUSILUKA ametoa rai kwa Vyuo vikuu Nchini kuandaa wanafunzi hasa katika sayansi ya matumizi ya akili mnemba ili kukabiliana na changamoto ya ajira pindi wanapomaliza elimu ya vyuo vikuu.

Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM, licha ya kuwa ni miongoni mwa vyuo vikuu vinavvyodahili idadi kubwa ya wanafunzi nchini pia kimekuwa moja ya taasisi kinara katika kutoa elimu ya matumizi ya akili mnemba.

Prof. Kusiluka ameyasema hayo leo Disemba 4,2024 wakati wa Kongamano la 15 la Wahitimu wa Chuo hicho, ambapo amesema katika zama hizi za sasa zinazohitaji uwekezaji wa kuisoma teknolojia Chuo Kikuu Cha Dodoma wenyewe wamekuwa kinara katika eneo hilo.

" Chuo Kikuu cha Dodoma tupo kwenye mchakato wa kuandaa miongozo inayoendana na Mazingira ya nchi yetu kwani teknolojia ya Marekani ni tofauti na ya Tanzania hivyo hatuwezi kuchukua moja kwa moja miongozo yao ni lazima tujiridhishe na hii teknolojia inayokuwa kwa kasi,

Na kuongeza kuwa " Imani yangu ni kuwa hadi kufikia mkutano mkuu wa 16 wa Umoja wa Wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dodoma 2025 tutakuwa tayari umekuja na miongozo ili kusaidia nchi katika maendeleo ya teknolojia," ameeleza Prof Kusiluka

Pia ametoa wito kwa Watanzania kutoichukia teknolojia bali waichukulie katika hali chanya huku wakitumia kwa faida kwani mabadiliko ya teknolojia yanakuja na changamoto zake ambazo ni vyema jamii ikaelimishwa ili isitumike na kuondoa ule Utanzania.

"Kikubwa hapa tunapaswa kutengeneza miongozo ambayo itatusaidia ni kwa namna gani teknolojia mpya ambazo hatuwezi kuepuka kuzitumia na tutazitumiaje kwa ajili ya kujenga kizazi chenye wasomi ambao wanatambua kwamba ni watanzania, lakini sio wasomi tu ambao wamejaza vitu vingi kichwani ambao hawajui kama ni watanzania ," amefafanua Prof Kusiluka

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwanza Prof. Flora Fabian ambaye pia ni mwanachama wa Umoja wa Wanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dodoma amewasilisha mada ya Ajira kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu katika kipindi hiki cha akili Mnemba na inakuja na changamoto gani na vyuo Vikuu vimejipangaje kuhakikisha wanaandaa wahitimu ambao wanakidhi katika soko la Ajira.

Ambapo amesema mada hiyo imelenga kuangalia ufundishaji na mashirikiano yaliyopo kati ya Vyuo Vikuu na Soko la ajira lenyewe Ikiwemo viwanda na sekta mbalimbali ambazo zinapokea wahitimu.

Amesema katika kipindi hiki cha akili Mnemba inaweza kuja na changamoto na inaweza pia kuja na faida zake kwa sababu akili Mnemba inatokana pia na akili za Binadamu.

" Binadamu ndio anatengeneza akili Mnemba hivyo kazi kubwa tuliyonayo vyuoni ni kuhakikisha tunazalisha wahitimu ambao ni wafikiriaji na Wabunifu ambao wanaweza kutumia hiyo akili Mnemba kutatua matatizo ya kijamii," amesema Prof Flora

Aidha wanazuoni hao wamesema ni muhimu vyuo vya elimu ya juu kuandaa wasomi watakao kabiliana na dunia ya sasa.

Chuo Kikuu cha Dodoma kipo katika mfululizo wa mahafali ya 15 kikianza na kongamano la kitaaluma.




No comments:

Post a Comment