RPC DODOMA APIGA MARUFUKU FATAKI SIKU YA SIKUKUU BILA KIBALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 23, 2024

RPC DODOMA APIGA MARUFUKU FATAKI SIKU YA SIKUKUU BILA KIBALI



Na Okuly Julius _DODOMA


JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limewahiza wananchi kujiepusha na upigaji wa fataki na baruti bila kibali wakati wa sikukuu kwa faida za usalama wao na watu wengine.

Hayo yamebainishwa leo Disemba 23,2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama mkoa wa Dodoma kuelekea sikukuu.

Amesema kipindi cha sikukuu mara nyingi huambatana na matukio ya ajali,ugomvi na matukio mengine yasiyofaa kutokana na ulevi uliopitiliza.

“Kuna tabia ambayo inazuka wakati wa sherehe watu wanajisahau wanakunywa pombe kupitiliza matokeo yake wanasababisha kuingia katika hatari ya kusabisha ajali ambazo nizakujitakia na kuvamiwa.

Ameongeza kuwa :”Tunatoa rai kwa wananchi wote kusherekea sikukuu kwa amani na utulivu.Kila mmoja ahakikishe anakunywa kwa kiasi na kwa wanaosafiri na madereva kuhakikisha wanaepuka matumizi ya vileo.

Katika hatua nyingiine Katabazi amesema katika operesheni waliyofanya wamekamata pikipiki 31 zinazozaniwa kuwa za wizi, bangi kilo 10, mirungi kilo 10, Tv, Radio na gari.

Amewalika wananchi kujitokeza kwa wingi kutambua mali hizo wakiwa na nyaraka halali.

“Tumefanikiwa kukamata kijana mmoja kati ya watatu waliokuwa wakisakwa na jeshi la polisi wakidhaniwa kuwa ni “panya road”. Tunaendelea kusisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi,”alisema







No comments:

Post a Comment