WAZEE DODOMA WALAANI UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, December 23, 2024

WAZEE DODOMA WALAANI UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU



Na Okuly Julius _Dodoma


Chama Cha Wanaume Wazee Mkoa wa Dodoma kimeungana na Serikali katika kulaani uharibifu wa Miundombinu ikiwemo ya Reli na Barabara unaofanywa na baadhi ya watu wenye nia OVU ya kurudisha juhudi za Serikali nyuma katika masuala ya Maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa leo Disemba 23,2024 na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dodoma Mzee PETER MAVUNDE wakati akieleza Mafanikio na Changamoto katika mwaka 2024 na matarajio ya Chama hicho mwaka 2025, ambapo amesema matukio ya uharibifu na wizi wa miundombinu ni matumizi mabaya ya Kodi za Wananchi .

"suala la uharibifu wa miundombinu sisi kama wazee hatuwezi kufumbia macho tunaungana na Serikali kulaani kwani wanaofanya hivyo Wanacheza na jasho la Watanzania ambalo ni kodi," ameeleza Mzee Mavunde

Pia Mzee Mavunde amezungumzia suala la Maadili katika jamii ambapo amesema changamoto za malezi mabovu ngazi ya familia ndio yanayosababisha matukio ya mmomonyoko wa maadili, hivyo akazitaka familia kufikiri upya katika suala Zima la Malezi.

"Malezi kwa sasa yamekuwa magumu Sana kwa sababu ngazi ya familia imeacha ule utamaduni wa kukemea makosa kuanzia ngazi ya msingi kabla ya Jamii kwani zamani sisi ukikosea mtu yeyote anaweza kukuadhibu na ukifika nyumbani kwenu bado unaadhibiwa maradufa ila kwa sasa ukimuadhibu mtoto wa mtu unaishia kwenye haki za binadamu ila tunaharibu kizazi kwa kwenda kinyume na utamaduni, " amesisitiza Mzee Mavunde

Pamoja na hayo Mzee Mavunde amewataka vijana kuwakumbuka wazee wao wasiwatelekeze kwani kufanya hivyo ni kujifungia Baraka ambazo wangezipata kwa kuwahudumia Wazee.

Naye Mzee Komredi Ntemo Mohamed amesema serikali ichukue hatua kali kwa wanaohujumu miundombinu huku akiwataka wazee kushiriki kikamilifu katika malezi

"tutakachokifanya wazee kwa sasa ni kwenda katika jamii na kutoa elimu juu ya Maadili na kuhamasisha wananchi kujikita katika malezi kuanzia ngazi ya msingi yaani familia kwani ndiko maandalizi ya mwanzo kabisa ya mtu yanapoanzia," Komredi Mohamed




No comments:

Post a Comment