Na Mwandishi Wetu, DODOMA
SERIKALI imesema haipendezwi na matamko ambayo yamekuwa yakitolewa na Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kwani baadhi yamekuwa na msukumo wa kisiasa na si kitaaluma.
Hivyo imeshauri chama hicho kutoa ushauri kwa njia bora zaidi huku wakizingatia taaluma zao.
Hayo yalibainishwa jijini Dodoma leo Disemba 16,2024 na Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Damas Ndumbalo mara baada ya kusaini makubaliano kati ya serikali na TLS katika masuala mbalimbali.
Amesema Duniani kote hakuna serikali inayo kubali kushushiwa heshima huku akisisitiza TLS kuzingatia miiko na maadili ya chama chao
"Kuna wakatiki unakutaka chama cha siasa kinatoa kauli hii dhidi ya serikali na TLS inakuja mbele ya vyombo vya habari inatoa kauli hiyo hiyo dhidi ya serikali maana yake hawa wote wako pamoja. Mimi nadhani kazi yenu ni kushauri serikali na sio lazima muendee katika vyombo vya habari,"amesema
Ameongeza kuwa;" Yale matamko ya mihemko hayafurahishi machoni pa serikali .Niwaombe tuendelee kushirikiana ili tuwahudumie Watanzania wapate elimu na msaada wa kisheria,"
Katika hatua nyingine Ndumbalo amesema hivi sasa serikali inaendelea kutoa msaada wa kisheria kupitia mama Samia legal aid campaign ambapo imeshafika katika Mikoa 11 na lengo ni kufika nchi nzima.
Amesema TLS ni kiungo muhimu katika kampeni hiyo kwasababu katika baadhi ya maeneo waliyopita wapo wanachama wa chama hicho ambao wameshiriki.
"Wanachama wa TLS tusiwe sababu ya kuleta migogoro serikali Ina mengi ya kushirikiana na ninyi na makubaliano haya ni ishara kuwa milango imefunguka,"amesema
Ameongeza kuwa :"Serikali inatoa gari kwa ajili ya kumsaidia shughuli mbalimbali za TLS na huu ni mwanzo Tunatamani kuona chama Hiki kunakuwa kama vyama vingine vya kitaaluma.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa TLS Laetitia Ntagazwa amesema chama hicho kimepewa jukumu la kushauri serikali, bunge na kuwatetea na kuwalinda wananchi.
"Niwahakikishie kuwa mashirikiano ambayo tumeingia leo si ya kuhongwa Wala kununuliwa na serikali bali ni kwa ajili ya kuongeza tija kwa manufaa ya umma wa Watanzania,"alisema
Ameongeza kuwa :"Kama vyama vya siasa vinapewa ruzuku na havijapewa jukumu la kusaidia Watanzania kwanini TLS isipewe Ili kuhakikisha inafikiwa wananchi wasio na uwezo wa kulipa mawakiki Ili haki zao za msingi ziweze kupatikana.

No comments:
Post a Comment