TOTO AFYA KADI KULETA MATUMAINI MAPYA NA UELEKEO WA NHIF - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, December 17, 2024

TOTO AFYA KADI KULETA MATUMAINI MAPYA NA UELEKEO WA NHIF



Na Okuly Julius _ Dodoma


Waziri wa Afya JENISTA MHAGAMA amesema kurejeshwa kwa Toto Afya Kadi kutaleta matumaini mapya na uelekeo thabiti wa Bima ya Afya hususani kwa kundi la watoto ambalo linahitaji uangalizi wa pekee huku akikemea tabia ya baadhi ya watoa huduma wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaotumia mfuko kujinufaisha.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati akizindua vifurushi vitatu vya vya Bima ya Afya kikiwepo cha Toto Afya Kadi ambapo amesema Mpango huo wa Toto Afya Kadi utasaidia familia za Wananchi hasa zile zenye watoto wenye changamoto za kiafya na utafanyika kwa mtoto mmoja mmoja ambaye atakuwa shuleni.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na UKIMWI ELIBARIKI KINGU ameishukuru Serikali kwa kutekeleza maagizo ya Bunge huku akiahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kulisemea suala la Bima ya Afya.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dakta IRENE ISAKA amesema kuzinduliwa kwa mfumo wa kidijitali kumewawezesha kushughulikia folio 1200 kwa dakika 45 tofauti na awali ambapo walishighulikia folio 800 tu kwa siku.

Naye, Mwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini EDGA GABRIEL amesema kuzinduliwa kutasaidia kutambua viashiria vya awali vya udanganyifu, hivyo wanaipongeza NHIF kwa ubunifu huo.

Mbali na kifurushi cha Toto Afya Kadi kilichozinduliwa leo, vifurushi vingine ni Ngorongoro chenye huduma 445 na Serengeti chenye huduma 1,815 ambavyo vyote vimelenga kuhudumia Watanzania.





No comments:

Post a Comment