Akizungumza katika kikao hicho kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt Catherine Joachim amesema kikao hicho kitawezesha kujadili na kuona ni namna gani watatifi hao wataweza kuweka mwendelezo wa tatifi na kujua kwa pamoja zimeweza kuleta matokeo yapi na kusaidia watunga sera kuzifanyia kazi.
“Kupitia kikao hiki tutaweka mikakati itakayowezesha kufanyika tafiti zaidi, ushirikiano katika kufanya tafiti ya kuweka njia zitakazorahisisha upatikanaji tafiti zote zilizofanyika nchini kuhusiana na VVU na UKIMWI.
Aidha ameongeza kuwa kikao hki kiwe ni chachu ya watafiti kufanya utafiti wao na kuweza kutumia tafiti hizo katika kufikisha nchi kuamini katika tafiti na kufanya maamuzi kwa kurtengemea tafiti zinazofanyika.
Dkt Catherine ameongeza kuwa TACAIDS imedhamiria kuwa na kikao cha wadau wote wa tafiti za VVU na UKIMWI nchini kila mwaka , na hii iwe fursa kwa wadau na watunga sera kuweza kupata matokeo kwa kupitia vikao kwa kupitia Desertation for HIV and AIDS Research paper findings ,kuanzia mwaka huu TACAIDS itaanza kutengeneza kanzidata ya tafiti zote zinazohusu masuala ya VVU na UKIMWI zilizofanyika nchini.
Aidha amebainisha kuwa huu ni mwanzo wa vikoa hivi vya watafiti ambapo kupitia kikao hiki tume itaandaa mikakati ya kufanya tafiti nyingi na zenye ubora zaidi kuweka mikakati ya ushirikiano na upashanaji habari na ufuatiliaji wa raslimali kwa ajili utafiti wa masuala yanayohusu VVU na UKIMWI.
Wataalam kutoka taasisi za utafiti walioshiriki katika kikao hicho wameshauri kuwepo kwa mfumo utakaowezesha kupatika kwa tafiti zote zilizofanyika katika eneo la HIV. Vikao vingine kama hivi vifanyike kila baada ya muda maalum na kwamba lugha ya uwasilishaji wa tafiti iwe ni ile nyepesi kueleweka hususan kwa watunga sera. Imependekezwa pia TACAIDS ihamasishe watafiti kuandaa muhtasari wa tafiti zao na kuziweka katika lugha nyepesi kueleweka kwa watumiaji.
Aidha kutokana na upungufu wa raslimali fedha katika Mwitikio wa UKIMWI, Serikali iongeze ufadhili katika maeneo ambayo hayafadhiliwi na wadau hususan yale yanayolenga kampeni za kutoa elimu.
TACAIDS kushirikiana na NIMR ili kupata
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka ofisi ya Serikali Bw. Elias Omar amewashukuru washirki wa mkutano huo kuwa huu ni mwanzo mzuri kwakuwa iwapo makubaliano waliyoyaweka kupitia kikao cha leo kitaosaidia mchango mkubwa kwa watunga sera mipango yao.
No comments:
Post a Comment